Unknown Unknown Author
Title: TANZANIA NA CHINA KUDHIBITI BIDHAA FEKI
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Shirika la Viwango Tanzania (TBS), limeingia mkataba na Serikali ya China kufanya ukaguzi na kudhibiti uingizwaji wa bidhaa feki nchini. ...
Shirika la Viwango Tanzania (TBS), limeingia mkataba na Serikali ya China kufanya ukaguzi na kudhibiti uingizwaji wa bidhaa feki nchini.
bidhaa feki
Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara, Mussa Uledi alisema jana kuwa China inatambua thamani ya ushirikiano wake kibiashara ndiyo maana imekubali mkataba huo wa ukaguzi.

“China wanatupa changamoto juu ya maendeleo yao na sisi Watanzania tuwajibike na kuwa wabunifu hususan katika kuongeza viwanda ili kuhakikisha nchi inaendelea kiuchumi,” alisema Uledi.

Alisema viwanda ndiyo msingi wa maendeleo ya nchi yoyote ile ndiyo maana hata wagombea wa nafasi za urais, ubunge na udiwani wanaweka kipaumbele sera ya kuongeza viwanda.

Mkurugenzi wa TBS, Agnes Mneney alisema Tanzania haina shaka na bidhaa zinazotoka China bali kuna wafanyabiashara wasio waaminifu wanaosambaza bidhaa feki.

“Bidhaa nyingi feki zinazoingia nchini kwa njia za panya ni vigumu kuzidhibiti, kwani mipaka yetu mingi iko wazi, japokuwa tunadhibiti maeneo ya bandari na uwanja wa ndege,” alisema Mneney.

Hata hivyo, alisema changamoto kubwa inatokana na uchache wa wafanyakazi wanaoshindwa kudhibiti maeneo yote, lakini Serikali imeongeza idadi ya watumishi ili kufanya kazi hiyo.

Alisema wanashirikiana na wananchi wanaotoa taarifa maeneo yenye bidhaa hizo.

About Author

Advertisement

 
Top