Unknown Unknown Author
Title: YANGA YAICHAPA COASTAL UNION BAO 2 - 0. MSUVA NA NGOMA HABARI YA MUJINI
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Wana jangwani Young Africans SC hii leo wamerudi kileleni mwa Ligi kuu bara Tanzania kama ilivyokua msimu uliopita baada ya kuilaza timu y...
Wana jangwani Young Africans SC hii leo wamerudi kileleni mwa Ligi kuu bara Tanzania kama ilivyokua msimu uliopita baada ya kuilaza timu ya Coastal Union kwa bao mbili kwa sufuri.
Saimon Msuva
Saimon Msuva aliiweka Yanga mbele mnamo dakika ya nane kisha raia wa Zimbabwe Donald Ngoma kufanya mambo kua 2-0 katika dakika ya 42 ambapo mchezo ulikua wa kusisimua sana.

Amissi Tambwe na Geoffrey Mwashiuya walipoteza nafasi za wazi wakati wa kipindi cha pili kilipoanza na kocha Han Van Der Pluijm akafanya mabadiliko. Malimi Busungu alichukua nafasi ya Amissi Tambwe huku Deus Kaseke akichukua nafasi ya Mwashiuya.

Patrick Protas wa Coastal alipoteza nafasi ya wazi ya kuifuta Coastal machozi dakika kadhaa baada ya kuingia uwanjani.


Yanga SC sasa ipo kileleni mwa Vodacom Premier League ya Tanzania bara.

About Author

Advertisement

 
Top