TAMASHA LA SIMBA DAY LAWA KIVUTIO , SIMBA YAITANDIKA SC VILLA KIMOKO 1-0

Simba Day
Wachezaji wa Simba wakitoka vyumbani kuingia Uwanjani
Simba Day
Kocha Mkuu wa Simba Kerry akiwa na kocha Msaidizi Seleman Matola
Simba Day
Hamis Kiiza'Diego' akitafuta mbinu za kumtoka beki wa Villa
Simba Day
Mussa Hasan Mgosi akiwa katika harakati za kugmbania mpira na beki wa Villla
Simba Day
Mashabiki wa Simba wakifuatilia mechi
Simba Day
Kikosi cha SC Villa ya Uganda

SIMBA Dar es Salaam.Simba inayonolewa na kocha kutoka Uingereza Dylan Kerr imeanza kuonyesha makeke yake baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhi ya timu SC Villa ya uganda katika mchezo wa kirafiki uliofanyika katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.

Simba licha ya kucheza kandanda la kuvutia ilibidi wasubiri hadi dakika ya 89, ambapo Awadhi Juma ndiye aliyenogesha sherehe za Simba baada ya kufunga bao hilo kufuatia shuti kali alilopangua kipa wa Villa na mpira kumkuta Awadhi.

Awali ulifanyika mchezo wa Viongozi wa Simba na timu ya wasanii ambapo timu ya viongozi walipata bao 1-0 bao lililofungwa na kocha Mkuu wa Simba Kerr.
Previous Post Next Post