Fenerbahce wamekubaliana mpango wa kumnunua Mchezaji wa Machester United Robin van Persie na amesain mkataba wa miaka minne, Taarifa hiyo ni kwa mujibu wa chanzo cha SkySport.

Robin van Persie
Klabu ya Uturuki sasa inamatumaini ya kutangaza rasmi uhamisho huo kabla ya mwishoni mwa wiki, lakini bado kuna baadhi ya maelezo ambayo yanahitaji kukamilika na kukubaliana na Van Persie mwenyewe.
Mkurugenzi wa Fenerbahce Guiliano Terraneo alisafiri hadi London hivi karibuni kujadili mpango wa uwezekano wa kusajili Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 31 wa timu ya taifa ya Uholanzi ambaye amebakiza mwaka mmoja katika mkataba wake Old Traffod, ingawa hadi sasa United bado haijasema chochote juu ya Deal hilo.
Tags
SPORTS NEWS