Watoto wa Kituo cha Huruma Foundation Mkoani Lindi wakiwa katika Futru mwishoni mwa wiki, iliyoandaliwa na Mfanya Biashara wa Hoteli ya M.M. iliyopo Manispaa ya Lindi Ndg: Hamza Mkurunga.

Sheikh Mkuu wa Mkoa wa lindi Mohamed Said Mushangani (kushoto) akiwa na Mmiliki wa Hoteli ya M.M Ndg: Hamza Mkurunga (kulia) katika hafla ya Kufuturisha watoto wanaolelewa na Kituo cha Huruma Founfation. Lindi. Haflahiyo ilifanyoka katika Ukumbi wa Hoteli hiyo ya M.M. wiki jana
Na.Abdulaziz Ahmeid, Lindi
Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Shekhe Mohamedi Saidi Mushangani, amewataka vijana kuishika elimu, kwani ndio njia pekee itakayowasaidia katika maisha yao ya baadae ili kukuwa wakitekeleza yaliyo mema kwa mujibu wa Taratibu za Dini.
Wito huo umetolewa mwishoni mwa wiki alipokuwa akizungumza na watoto wa kituo cha Huruma Foundation cha Manispaa ya Lindi, katika hafla ya kufuturisha iliyofanywa na Mfanyabiashara aitwae Hamza Mkungura, anayemiliki nyumba ya kulala wageini iitwayo M M Hotel iliyopo mjini humo.

Sambamba na Futari hiyo Sheikh Mushangani amewasisitiza vijana kutumia umri walionao kujikita kwenye masuala ya masomo,kwani urithi pekee utakaowasaidia maisha yao ni elimu,ikwemo ya Dini ili kumcha vema mwenyezimungu.
Aidha amewataka watoto hao kujenga tabia ya kuwaheshimu viongozi wa taasisi hiyo ya Huruma Foundation,pamoja na walimu wao ili waweze kupata elimu itakayowasaidia katika maisha yao ya baadae.
“Msipowaheshimu walimu,elimu kichwani mwenu haitakuweza kuwai ngia, hivyo ninawasisitiza jitahidini kuwaheshimu” Alisisitiza Shekhe Mushangani.
Amesema kutokana na majukumu wanayoyatekeleza, walimu na madaktari ni miongoni mwa wataalamu wanaohitajika kuheshimiwa na kupewa hadhi ya msingi.
Kiongozi huyo amesema walimu na madaktari wasipoheshimiwa na kutunzwa ni hasara kubwa, mbele ya jamii, kwani hawataweza kutekeleza vema majukumu yao kwa wananchi, wakiwemo watoto katika kuwapa elimu iliyo bora.
Hasani Chunusi meneja wa Hoteli hiyo iitwayo Double M, ameupongeza uongozi wa kituo cha Huruma Foundation kwa kuweza kukubali mwaliko wao, huku akiwasisitiza vijana hao kutumia muda walionao kuongeza kasi katika elimu.
Mkurugenzi wa Hotel hiyo, Hamza Hassani Mkungura, alisema mwaliko alioufanya wa kuwafutulisha vijana hao, ni sehemu ya faida wanayoipata kutoka kwa wazazi na wazazi wao wanaofika Hotelini hapo kuchangia kupatiwa huduma mbalimbali, ikiwemo chakula na malazi.
Naye, kiongozi wa kituo hicho cha Huruma Foundation, Halima Mbalijika, amempongeza mfanyabiashara huyo kwa moyo wa upendo aliounyesha zidi ya watoto hao, huku akiomba wengine kuiga mfano wake.

Watoto wanaolelewa na kituoa cha Huruma Faoundation wakiwa katika mazungumzo kabla ya Futru iliyoandaliwa kwa ajili yao na mmiliki wa hoteli ya M.M Ndg Hamza Mkurunga mwishoni mwa wiki.

Watoto wanaolelewa na kituoa cha Huruma Faoundation wakiwa katika Ukumbi wa MM Hotel kupata futru iliyoandaliwa kwa ajili yao na mmiliki wa hoteli hiyo Ndg Hamza Mkurunga mwishoni mwa wiki.

Ndg Hassani Chunusi Meneja wa Hoteli ya M.M akiwahudumia watoto wa kituo cha Huruma Faoundation katika Ukumbi wa M.M Hotel wakati wakupata futru iliyoandaliwa kwa ajili yao na mmiliki wa hoteli hiyo Ndg Hamza Mkurunga mwishoni mwa wiki.