BELA AHOFIA MAISHA YAKE, BAADA YA KUANDAMWA KWA VIPIGO MFULULIZO, SABABU ZOTE ZIKO HAPA

Msanii wa Kizazi kipya na Pia muigizaji wa Filam Nchini Tanzania anayefahamika kwa jina la Isabela Mpanda (@belafasta) ameweza kuelezea wasi wasi wake wa maisha yake kwa kile alicchokisema kuwa kinasababishwa na Msanii mwenza wa Mchumba wake Letuni Karama ambaye wapo wote katika kundi la Gangwe Mob.
Isabela Mpanda
Bela amefunguka hayo yote kupitia Ukurasa wake wa Mtandao mmoja wa kijamii na kueleza kinaga ubaga nini kilichomkuta, Na hichi ndicho alichokiandika:-
"Kuna siku tulikua tuna show mara majamaa watatu waka nivamia wakaanza kusema we dem leo tuna kupadua uwez kumzuia @lutenkarama asifanye mzik wala show .wale watu wakaanza kunivuta uzur karama alikua pemben anaongea na watu akaona mbona bela anavutwa?ndo akaja kuwapoza washkaj akawauliza vp wakasema mwenzio anasema uyu dem atak ww ufanye kaz ndo maana tumekasirika sisi tunapenda gangwe mobb iweje uyu dem akuzuie? karama aka waelewesha yaka isha. juz nipo na kina shub na ray tulienda sehem tuna ingia tu mlangon mtu simjui mtu mzima kanivuta kanipiga uku akisema wewe bela una mkataza karama asifanye show wala kaz mwenzie kaniambia apo ananipiga uku ana tukana. siku iliyo fuata natoka nje ya geti kwangu watu 3 wana tukana wanataka kunipiga uku wanasema wewe bela unaua gangwe unamzuia karama asifanye kaz . uzur kulikua na watu waliamua. jamani kweli uyu ni mtu mzuri?anafanya adi mimi nachukiwa na watu kisa afanye show peke yake. kuna siku mtu tupo nae mi na karama kampigia sim .oya kuna show naitaka gangwe apo apo akajibu nitakuja mimi tuu karama atak kaz dem kambana yeye ataki. jaman kumbuken apo kawekwa loud spika. MIMI NAWEZA ULIWA KISA SUMU ANAE NIPAKAZIA .NINA WAKATI MGUM SANA NA NDIYO MAANA NIMEAMUA KUWEKA WAZ.
Previous Post Next Post