MSHALE WA MLIMA ILULU:: HAITAKUWA AJABU MWENYE NGUVU KUSALIMU AMRI KWA MTUKUTU

Na.Ahmad Mmow.
Wapendwa mnao soma maandishi yangu. Pole kwa uchovu ulitokana na pilika pilika za kutafuta riziki au mkate wa kila siku. Mbarikiwe sana wapendwa. Ahsante kwa kusoma maandiko yangu, sina cha kuwalipa. Bali nawaombea kwa Mungu ninaye muamini aendelee kuwapa uzima na afya tele. 
CCM Lindi
Wapendwa, leo nitaanza kuwasimulia kisa cha kweli kilichofanyika miaka ya 1970, wakati ambao mimi nilikuwa bado mtoto nikiwa madarasa ya chini katika shule ya msingi. Msitake niwaambie ni shule gani niliyosoma. Kama mnaona ni muhimu niulizeni kwa wakati wenu.
Pale shuleni palikuwa na mwanafunzi mwenzetu mtukutu sana, sielewi yupo wapi sasa. Nakama yupo hai, naamini atakuwa ni mzee wa makamo sasa. Maana mimi nikiwa mtoto, yeye alikuwa kijana hasa. Nikaka yangu aliyenizidi miaka mingi.Kaka yangu huyo ambaye alikuwa mwanafunzi wa madara ya juu kuliko mimi alikuwa mkorofi sana. 
Hakuwa na nguvu na mjuzi wa kupigana kama kuwazidi wengine warika na makamo yake. Bali alikuwa anaogopwa na wanafunzi wote pamoja na waalimu. Sifa yake kubwa ni uvumilivu. Alikuwa hajali kupigana na wanafunzi wenzake walau mara tatu kwa kutwa. Ukisikia mayowe wanafunzi wakishangalia kwamaneno ngumiiii, ngumiii ukienda utamkuta yupo kibaruani anachapana na mwanafunzi mwenzake. Sifa yake kubwa ni uvulivu. Sijapata kuona mtu mvumilivu kama yule. Wewe mpige kadri unavyoweza, jamaa hakimbii anakuja tu. Utampiga mpaka unachoka, na ukichoka ndipo anapokushugulikia kisawasawa.
Siyo mara moja wala mbili nilishuhudia wababe wanaamua kumkimbia na wengine kuomba msaada wamuondoe ili kibao kisiwageukie. Wababe wengini waliishi kulia, baada ya kuona wamempiga hadi wanaishiwa nguvu wakati jamaa amevimba sura lakini bado akiwa fiti na ndiyo kwanza anaonesha hajachoka. Ungekuwa wewe ungefanyaje zaidi ya kulia au kutimua mbio?
Kutokana na sifa hiyo aligeuka kuwa mbambe hata kwa wale tuliowaamini walimzidi nguvu. Aliweza kufanya chochote alichotaka. Ikiwa ni pamoja kuchukua kwa nguvu chochote alichotaka. Kisa hicho nimekikumbuka baada ya kumlinganisha mtangazania mmoja wa urais ambaye kwasasa sitamtaja. Na kwamila zetu wangindo huwa hatujanitajani majina kwenye visa vya aina hii. Wenyewe kingindo tunaita unhwilo(mwiko) kwani madhara yake ni makubwa. Namimi nimiongoni mwa wanaoheshimu sana mila za kwa kwetu. Mtangaza nia huyu ameanza kugeuka mbambe kama ilivyokuwa kwa mwanafunzi kaka yangu wa enzi zile shuleni. Wenye nguvu ikiwamo viongozi wa chama chake walianza kupambana nae kiasi cha kutaka kumfukuza uanachama wa chama chao. Lakini aliwagomea na akasababisha baadhi rafiki zake watukutu kuungana nae katika mgomo. Viongozi wakanywea na kubaki kumtazama macho huku wakilalama kwa kujipa matumaini kwamba ipo siku watamtandika. Hakuwajali wala kutishika na mikwala yao. Aliendele kufanya fujo kwa kwenda mbele na kujizolea mashabiki na wafuasi kibao. Miongoni mwao waliamua kujisalimisha kwake wakiamini siku moja kwa kutumia ubabe wake watafaidika. Wengine wamejisalimisha kutokana na woga tu, baada ya kubaini hawezekani na hakuna atayemmudu tena. Hali imebadilika, sasa amejizolea wafuasi wanaomuunga mkono na kumshangilia. 
Sasa anakitaka cheo cha juu kabisa cha uongozi wa nchi. Wanapiga kelele na anashambuliwa kila kona, kama mwanafunzi yule mtukutu ambaye aligeuka kuwa mbabe. Hasikii wala hajali, yeye anasonga mbele tena kwakasi kubwa kweli ambayo viongozi wa chama chake kama ilivyokuwa kwa waalimu wa shule ile walivyokuwa wamechanganyikiwa na mwanafunzi yule, ndivyo walivyo changanyikiwa. Hawajui wafanye nini ilikumzua asichukue anachokihitaji. Mtukutu alivyang'anya vitu vidogovidogo vya wanafunzi wenzake na vya shule, sasa anapambana kuingia stoo akahamishe kila kilichomo humo.
Viongozi wa chama chake wamechanganyikiwa wasijue la kufanya zaidi ya vitisho ambavyo huku kwetu tunaviita mikwala. Na yeye anajua kwamba hawamuwezi tena, na kwamba wanachofanya ni mkwala na mwisho wa siku watachemka. Kama viongozi wake chama wange kuwa na uwezo wangemdhibiti mapema. Walimuita gamba na wakataka kumfukuza chama, lakini alifokea kama ilivyokuwa kwa mwanafunzi yule kwa walimu wake ambao mwisho wa siku walinywea. Mara hii amepata wafuasi na waungaji mkono wengi wanamshangili kila anapopita. Watamuweza kweli! Nadhani nikama waalimu wa siku zile walivyokuwa wanachungulia kupitia madirishani wakati mtukutu anafanya vitu vyake.
Ndipo napata mashaka kwamba kwa kasi ya mtangazania huyu viongozi wa chama chake kazi wanayo mwaka huu. Jamaa ni shiiida kweli kweli. Viongozi wa chama wanahema juujuu kwa hofu kwani jamaa anakuja kama dhuruba ya stunami. Kateni jina lake muone kimbembe, pitisheni muone ghazabu na hasira za umma.
Naamini wananchi hawatashindwa kumshugulikia. Wanaomshangalia na kumuunga mkono siyo wananchi wote. Wengine wanahasira nae. Mkipitisha watapigia mpira kwenye michongona. Mkimkata mjue yeye na wafuasi wake watapigia pira kwenye misumari. Patamu hapo! Uchimeche wala uchiteme. Ukimecha nchale, ukitema nchale na umung'anya nchale.Duh! Naukumbuka wimbo wa bendi ya mlimani paki ulikuwa unamalizia kwa ohoo mama najutae ohoo mama nifanye nini, mambo yamenikuta mwenzenu yamenikuta! Hapa mwenye nguvu atalia. Kama mnabisha subirini tuone. Yetu macho namasikio. Tutaonana siku nyingine.
Previous Post Next Post