
Mufti Sheikh Issa Shaaban Bin Simba (Enzi za Uhai wake) akiwa na Mh. Rais Jakaya Kikwete
Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Sheikh Alhadi Mussa Salum nimemnukuu akithibitisha juu ya msiba huo “Ni kweli Mheshimiwa Mufti amefariki.. Kesho saa nne asubuhi Waislamu na Viongozi wote watajumuika Makao Makuu ya BAKWATA, Kinondoni Muslim kuuaga mwili wa Sheikh. Mchana mwili wa Sheikh utasafirishwa kwenda Shinyanga, atazikwa siku ya Alhamisi" Sheikh Alhadi Mussa Salum
Hapa anamzungumzia Marehemu Mufti Simba “Mufti alikuwa na sifa ya kuwa Kiongozi wa Waislamu. Alikuwa mvumilivu sana na msamehevu katika Utawala wake. Angekuwa hana subira Waislamu wasingekuwa na uvumilivu" Sheikh Alhadi Mussa Salum.
Bonyeza play hapa chini kusikiliza live...
Tags
HABARI ZA KITAIFA