CRISTIANO RONALDO AKANUSHA TAARIFA ZA YEYE KUONDOKA REAL MADRID, ASEMA ANAFURAHA SANA NDANI YA CLUB HIYO

Mchezaji wa Dunia wa Mwaka, Cristiano Ronaldo amevunja ukimya baada ya miezi kadhaa ya minong'ono ya vyombo vya habari kuwa yeye hana Furaha na Club yake ya sasa ya Real na kuwa inawezekana anatafuta njia ya kutoka.
Cristiano Ronaldo
Cristiano Ronaldo kwa sas yupo Miami katika mapumziko ya likizo yake.

Mshambuliaji huyo wa kireno alifanya kauli yoyote kuwa na ugumu hasa pale alipowaambia waandishi wa habari baada ya mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Schalke 04 mwezi March, kuwa hataki kuzungumzia suala hilo hadi mwisho wa Msimu.

Pamoja na jitihada zake za ufungaji wa Magoli, real walimaliza msimu bila ya kuwa na Kikombe hata kimoja, matokeo hayo yalipelekea Kocha Carlo Ancelotti kufutwa kazi na kuletwa kocha mpya Rafa Benitez.

Mchezaji huyo wa Zamani wa Manchester United alitegemewa kuondoka clubuni hapo hasa baada ya kuonesha kuumizwa kwa kufunkuzwa kwa kocha Ancelotti na Ujio mpya wa Kocha Benitez ambao umefanywa na Rais wa Club hiyo Florentino Perez.
Cristiano Ronaldo
Cristiano Ronaldo akichezea Mpira wa mchezo wa beach, kwa sas yupo Miami katika mapumziko ya likizo yake.

"Napenda kuwaambia watoa taarifa za uongo kuacha maramoja, ili niachwe na amani" alisema Ronaldo ambaye yupo katika likizo katika Mji wa Miami.

"Taarifa ya Kwamba mimi nilitaka kujenga Mgogoro kati yangu na Real Madrid ni ya uongo kabisa"

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30 alinukuliwa akisema hayo na gazeti la michezo la Kireno "A BOLA" siku ya Jumamosi.

"Ninafuraha sana katika klabu yangu bora duniani na niko makini sana na Ujasiri wa msimu mpya wenye mafanikio."
Previous Post Next Post