NI HUZUNI TENA NDANI YA BONGO MOVIE KWA KIFO HICHI. WASANII WAJAWA NA MAJONZI TELE...!!!

Mazishi ya Baba wa Steve Nyerere
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda akiweka shada la maua kwenye kaburi la marehemu Francis Festus Mengele.
Mazishi ya Baba wa Steve Nyerere
Shangazi wa Msanii, Steve Nyerere, Grace Mengele (katikati), akiwa na wadogo zake Steve Nyerere wakati akiwasili makaburi ya Kinondoni kwa mazishi ya mpendwa wao, Francis Mengele.

Na Dotto Mwaibale
WASANII mbalimbali wa filamu na bongo fleva wamejitokeza kwa wingi katika mazishi ya baba ya msanii mwenzao Steve Mengele 'Steve Nyerere, aliyofanyika juzi makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Msanii Jacob Stephen JB ni miongoni mwa wasanii waliohudhuria mazishi ya marehemu Francis Mengele baba yake na msanii huyo aliyefariki wiki iliyopita kutokana na maradhi ya mapafu.
Wasanii wengine waliohudhuria mazishi hayo ni pamoja na Micky, Vicent Kigosi 'Ray' Elizabeth Michael 'Lulu', Chuchu Hans, Kajala Masanja 'Kajala' , Mtunzi na muongozaji wa filamu Myovela Mswaisa na wengine wengi.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda aliyeongoza mazishi hayo alisema kifo cha Mengele ni pigo kubwa katika wilaya hiyo ya Kinondoni na familia kwa ujumla.
"Mengele alikuwa na mchango mkubwa katika wilaya yetu ya Kinondoni katika kulipa kodi kutokana na biashara zake alizokuwa akizifanya na wingi huu wa watu waliojitokeza katika mazishi yake inaonesha jinsi alivyokuwa akishirikiana na wenzake hasa waumini wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Usharika wa Kimara alikokuwa akisali" alisema Makonda.

Makonda alitumia fursa hiyo kuiomba Manispaa ya Kinondoni ndani ya miezi mitatu kuhakikisha inajenga choo katika makaburi hayo ya Kinondoni kwani ni aibu kwa eneo hilo kukosa choo hivyo kuwafanya wananchi wanaofika kwa ajili ya maziko kukosa huduma ya choo.
(Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com-0712-727062)

Mazishi ya Baba wa Steve Nyerere
Ibada ya maziko ikiendelea.
Mazishi ya Baba wa Steve Nyerere
Hali ilivyokuwa wakati wa mazishi.
Mazishi ya Baba wa Steve Nyerere
Waombolezaji wakijitayarisha kushusha jeneza lenye mwili wa marehemu.
Mazishi ya Baba wa Steve Nyerere
Jeneza likiwa limeshushwa kaburini.
Mazishi ya Baba wa Steve Nyerere
Ni huzuni tupu.
Mazishi ya Baba wa Steve Nyerere
Wasanii mbalimbali wakiume wakiwa kwenye mazishi hayo.
Mazishi ya Baba wa Steve Nyerere
Wasanii mbalimbali wakike wakiwa kwenye maziko hayo.
Mazishi ya Baba wa Steve Nyerere
Kaburi likijengwa baada ya kuwekwa mwili wa marehemu kaburini.
Previous Post Next Post