Viongozi wa vyama vya siasa wilayani Nachingwea mkoani lindi wametakiwa kuwa mstari wa mbele katika kuwaelimisha wa wananchi juu ya umuhimu wa kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura, pamoja na kushiriki katika zoezi la kuipigia kura rasimu ya katiba inayopendekezwa.
Wito huo umetolewa na waziri wa mambo ya ndani ya nchi na mbunge wa jimbo la nachingwea mathias chikawe wakati akikabidhi jumla ya pikipiki thelathini na mbili kwa makatibu kata wa chama cha mapinduzi wilayani humo, zenye thamani ya shilingi milioni hamsini na tano, ambapo pia amewataka makatibu hao kutumia usafiri huo kwa ajili ya kuwafikia wananchi na kuwaelimisha juu ya umuhimu wa kushiriki katika zoezi la kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura pamoja na uhamasishaji wa wananchi kushiriki katika zoezi la kuipigia kura rasimu ya katiba pendekezwa
Aidha, katibu mkuu wa ccm wilayani humo mussa rashid lilio amesema pikipiki hizo zitasaidia kwa kiasi kikubwa uelimishaji wa wananchi juu ya umuhimu wa uandikishwaji wa daftari la kudumu la wapiga kura pamoja na umuhimu wa kupigia kura rasimu ya katiba pendekezwa.
Kwa upande wao makatibu kata wa ccm waliokabidhiwa vyombo hivyo wamemshukuru mbunge chikawe kwa msaada huo huku wakiahidi kutumia usafiri huo kwa malengo yaliyokusudiwa.

Post a Comment Blogger Facebook
Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii
Note: Only a member of this blog may post a comment.