Mkuu wa Mkoa wa Lindi MWANTUMU MAHIZA, amewataka Wafanyabiashara Mkoani humo kuachana na tabia ya kufanya migomo na kufunga Biashara zao kwani kitendo hicho kina athiri kwa kiasi kikubwa Uchumi na Maendeleo ya Mkoa huo.
MWANTUMU ameyasema hayo alipokutana na Wafanyabiashara Mkoani humo kuzungumzia changamoto mbalimbali zinazowakabili wafanyabiashara hao kwa nia ya kuzipatia ufumbuzi ambapo amewataka wafanyabiashara hao kutojenga mazoea ya kufuata mkumbo wa kufanya Migomo kwani tabia hiyo inaathiri kwa kiasi kikubwa Maendeleo na Ustawi wa Wafanyabiashara hususani Wajasiriamali Wadogo Mkoani humo na hivyo kurudisha nyuma Maendeleo ya Mkoa huo.
Aidha Mkuu huyo wa Mkoa amewataka wafanyabiashara hao kutumia fursa za Kiuchumi zilizopo Mkoani humo kuwekeza badala ya kusubiria wawekezaji kutoka nje ya Mkoa huo.
MWANTUMU MAHIZA MKUU WA MKOA WA LINDI
Aidha Mkuu huyo wa Mkoa amewataka wafanyabiashara hao kutumia fursa za Kiuchumi zilizopo Mkoani humo kuwekeza badala ya kusubiria wawekezaji kutoka nje ya Mkoa huo.
Post a Comment Blogger Facebook
Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii
Note: Only a member of this blog may post a comment.