Unknown Unknown Author
Title: VURUGU ZATAWALA UWANJA WA ILULU MECHI KATI YA MARKETI PLACE FC Vs TIMBALAND FC
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Shabiki wa Timu ya Timbaland Fc ambaye hakuweza kupatikana jinalake mara moja akiwa Chini amepoteza fahamu mara baada ya kupigwa. Na...
Shabiki wa Timu ya Timbaland Fc ambaye hakuweza kupatikana jinalake mara moja akiwa Chini amepoteza fahamu mara baada ya kupigwa.

Na.Mwandishi Wetu, Lindi
Leo katika Mchezo wa Kwanza wa fainali ya Ligi daraja la Kwanza kati ya Market Place ya Mjini Lindi na Timu ya Timbaland ya Kutoka wilaya ya Nanchingwea Imekwishwa kwa Mashabiki kuoneshana ubabe ambao ulipelekea wengine Kuumizwa Vibaya huku Mechi hiyo ikiisha kwa Timu ya Market Place kuibuka Bingwa wa Mchezo huo kwa magoli 2 - 0.

Mashabiki wa Timbaland ndio walikuwa wakwanza kuonesha ubabe hasa kuanzia kipindi cha pili pale mpira ulipochelewa kuanza kwa kuwa mwamuzi wa mchezo huo alihitaji kuona vyombo vya ulinzi na usalama vikiwa uwanjani hapo kutimiza majukumu yao ya kulinda amani ya watu waliomo uwanjani humo.

Baada ya Mpira kuanza walionekana mara kadhaa kupinga maamuzi ya refa hadi kufikia kuaanza kuwazonga washika vibendera lakini Viongozi na Askari waliokuwa hawana sare za Jeshi la polisi waliokuwa wako ndani ya uwanja huo walilazimika kuwatuliza mashabiki hao. Lakini hali ilizidi kuwa si nzuri pale Marketi place Fc walivyo pata Goli la pili ambalo kwa mujibu wao waliona ilikuwa ni Offside lakini Mwamuzi wa pembeni hakunyoosha kuashiria mchezaji wa Marketi kuwa ameotea na Refa alilibariki kuwa ni goli halali kwa upande wa Timu hiyo ya wauza Nyanya ya Soko kuu la Mjini hapa.

Hali ya Sintofahamu ilihamia katika Jukwaa Moja la Upande wa Kulia mwa Uwanja huo ambalo hukaliwa na mashabiki wa Market Place, Shabiki mmoja wa Timbaland alijeruhiwa na kuweza kupoteza fahamu na ikabidi akimbizwe Hospitali kwa matibabu zaidi.

Hizi ni Baadhi ya Picha zikieleza Tukio Hilo.
Tukio Lilianzia Hapa Mashabiki wa Market Place Fc wakiwa jukwaani na Timbaland Fc wakilisogelea jukwaa hilo, Aliye wekewa Duara alisemekana ndie aliye mpiga shabiki wa Timbaland. 
Mashabiki wa Timbaland (miduara ya Blue) wakipanda Jukwaani kumfuata Shabiki wa Market Place (duara la Pink) aliye kuwa amekaa jukwaa hilo, ambae wanadai kuwa ndie aliye mpiga mwenzao. 
Mashabiki wakiwa Timbaland (Mishale ikionesha) wamemzunguka Shabiki wa Market Place wakitaka nae apigwe kwani walikuwa wamevua mikanda na kuanza kurusha huku watu wengine wakionekana kuwazuia wakidai huyo sie aliyefanya tukio hilo. 
Mashabiki wa Timbaland Fc wakiwa Nje ya Jengo lililo nje ya uwanja wa Ilulu wakitaka Shabiki wa Market Place atolewe nje nae apate kichapo, Lakini Polisi waliweza kumtoa mtu huyo na kuweza kuondoka nae.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top