Unknown Unknown Author
Title: MATOKEO YA MECHI ZA LEO LIGI KUU YA UINGELEZA HAYA HAPA: LIVERPOOL YAPOKEA KICHAPO NYUMBANI, CHELSEA IKINUSURIKA KUTOA DRAW
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Wakicheza Uwanjani kwa Mahasimu zao wakubwa huko Anfield Manchester United hii Leo wakishuhudiwa na Mfalme wa Soka Duniani, Pele , waliit...
Juan Mata
Wakicheza Uwanjani kwa Mahasimu zao wakubwa huko Anfield Manchester United hii Leo wakishuhudiwa na Mfalme wa Soka Duniani, Pele, waliitwanga Liverpool Bao 2-1 na kujishindilia Nafasi ya 3 ya Ligi Kuu England.
Juan Mata
Bao zote za Man United zilifungwa na Juan Mata Dakika za 14 na 59 na Bao la Liverpool likipatikana Dakika ya 69 kupitia Daniel Sturridge huku pia Kepteni Wayne Rooney akikosa Penati Dakika za Majeruhi.
Daniel Sturridge
Tukio jingine kubwa la mtanange huu ni kupewa Kadi Nyekundu kwa Nahodha wa Liverpool Steven Gerard Sekunde 38 tu baada ya kuingizwa kutoka Benchi mwanzoni mwa Kipindi cha Pili huku Man United wakiwa 1'0 mbele pale alipomtimba Anders Herrera.
Steven Gerard

PELE
Gwiji la Soka PELE akiwa ndani ya Anfield kutazama mtanange wa Liverpool Vs Manchester United

VIKOSI: Liverpool: Mignolet; Can, Skrtel, Sakho; Sterling, Henderson, Allen, Moreno; Lallana, Sturridge, Coutinho

Akiba: Jones, Johnson, Toure, Gerrard, Lambert, Lucas, Balotelli.

Manchester United: De Gea; Valencia, Smalling, Jones, Blind; Mata, Carrick, Ander Herrera, Young; Fellaini; Rooney.

Akiba: Da Silva, Rojo, Di Maria, Falcao, Januzaj, Valdes, Pereira.
REFA: Martin Atkinson

HULL CITY 2 - 3 CHELSEA
Eden Hazard
VINARA wa Ligi Kuu England Chelsea Leo nusura wakose ushindi ugenini na Hull City baada ya kuongoza 2-0 na kuiruhusu Hull kusawazisha na Gemu kuwa 2-2 lakini Loic Remy alitoka Benchi na kuja kuwapa ushindi wa Bao 3-2.
Ahmed El Mohamady
Ushindi huu umeifanya Chelsea izidi kuongoza Ligi ikiwa Pointi 6 mbele ya Mabingwa Watetezi Man City lakini pia Chelsea wana Mechi 1 mkononi.

Katika Mechi yao Leo, Bao za Chelsea zilifungwa na Eden Hazard Dakika ya 2 na DiegobCosta Dakika ya 9 huku Hull wakifunga Dakika za 26 na 28 kupitia Ahmed El Mohamady na Hernandez.
Loic Remy
Bao la ushindi la Chelsea lilifungwa na Loic Remy alieingizwa kumbadili Diego Costa na kupachika Bao lake Dakika ya 77.

EVERTON 2 - 1 QPR
Kwenye Mechi nyingine ya Ligi Kuu England iliyochezwa Leo huko Loftus Road Everton iliichapa QPR Bao 2-1.
Seamus Coleman
Bao za Everton zilufungwa Dakika za 18 na 77 na Seamus Coleman na Aaron Lennon likiwa Bao lake la kwanza kwa Everton tangu atue hapo kutoka Spurs.

LIGI KUU ENGLAND:: Msimamo-Timu za Juu

1. Chelsea Mechi 29 Pointi 67

2. Man City Mechi 30 Pointi 61

3. Arsenal Mechi 30 Pointi 60

4. Man United Mechi 30 Pointi 59

5. Liverpool Mechi 30 Pointi 54

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top