KIUNGO WA MANCHESTER UNITED MICHAEL CARRICK AMEONGEZA MKATABA WA MWAKA MMOJA

Kiungo mwenye Umri wa miaka 33 amekuwa katika fomu ya kuvutia kwa ajili ya Mashetani Wekundu hao hasa Mwishoni mwa wiki iliyopita alipoisaidia Timu yake hiyo kushinda dhidi 3-0 dhidi ya klabu yake ya zamani Spurs.
Micheal Carrik
Michael Carrick ameweza kusaini mkataba mpya wa mwaka mmoja na Manchester United. Kiungo huyu wa Kiingereza 33, mkataba wake ulikuwa unaisha mwishoni mwa msimu lakini amekubali kusaini Mkataba mpya wa miezi 12.

Kocha wa United Louis Van Gaal alisema: "Yeye ni muhimu kwa sababu anaweza kusoma mchezo, kama mchezaji uwanjani."Kwa hiyo anaweza kukochi wakati wa mchezo. Lakini anaweza kuboresha kiwango nadhani". Yeye pia ni mchezaji ambaye anaweza kupeleka mpira mbele kitu ambacho ninakipenda, kwa sababu lengoletu daima ni kuona mpira unakwenda mbele kuliko nyuma".

"Yeye ni nahodha wa pili kwangu hivyo ni mtu muhimu kwa ajili ya uteuzi wangu."
fellain Cerebration
United  watakutana na Liverpool katika uwanja wa Anfield siku ya Jumapili na Van Gaal , ambaye hajawahi hapo kabla, 
Rooney Cerebration
Alisema: "mechi ijayo ni dhidi ya Liverpool, na kwamba si ardhi ambapo Manchester United imeshinda Mechi nyingi."

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post