
Ajali hiyo ya kusikitisha imetokea leo saa 1.32 asubuhi katika barabara kuu ya Singida-Dodoma eneo la kijiji cha Isuna tarafa ya Ikungi wilaya ya Ikungi mkoani Singida.

Kamanda wa polisi mkoa wa Singida, SACP , Geofrey Kamwela, amesema gari hilo aina ya Noah lilikuwa likitokea Itigi wilaya ya Manyoni na lilikuwa na safari ya kuja Singida mjini.

Amesema hadi sasa miili ya abiria 10 wamekwisha tambuliwa na ndugu zao na miili ya abiria watatu, bado haijatambuliwa na miili yote bado imehifadhiwa kwenye chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali ya mkoa mjini Singida
Tags
HABARI ZA KITAIFA