
Hapo jana tarehe 07/02/2015 majira ya Saa 11.50 usiku Askari polisi wa Kizuizi cha Nangurukuru wakiwa katika Doria walifanikiwa kulikamata Gari lenye Namba za usajili UAU 789 Z likiwa na Madawa ya Kulevya aina ya HEROINE zinazokadiriwa kuwa Kilo 40 zikiwa zimehifadhiwa Ndani ya Gari hilo kwenye Paketi 40 zenye ujazo wa Kilo moja Kila moja.
Watuhumiwa wanaoshikiliwa na Polisi ni TUKURE ALLY, (55yrs) kabila Nyakole Dini Muislam Rais wa Uganda, wapili ni Sano Sadiki Abubakari (53yrs) Kabila Mandunguu Dini Muislam Mkazi wa Kampala Raia wa Gunie. Watuhumiwa hao wanashikiliwa na Jeshi la Polisi.
Tags
HABARI ZA KITAIFA