Timu ya taifa ya Ivory Coast iliyotwaa kombe la mabingwa wa Afrika, AFCON 2015, imepokelewa na mamia kwa maelfu ya mashabiki waliokusanyika kwenye uwanja wa ndege na mitaa mbalimbali ya mji mkuu wa kibiashara wa nchi hiyo Abidjan kuwakaribisha nyumbani.

Rais wa Ivory Coast Alassane Outtara alitangaza siku ya Jumatatu kuwa ya mapumziko kufuatia ushindi wa Ivory Coast kwenye fainali dhidi ya Ghana nchini Equatorial Guinea.






Tags
SPORTS NEWS