BREAKING NEWS: MOTO MKUBWA JIJINI DAR WAUNGUZA GHOROFA!

Ajali ya moto
Moshi mkubwa ukiwa umetanda katika paa la jengo hilo lililopo katika mtaa wa Jamhuri jijini Dar.

Dar es Salaam, Tanzania. Moto mkubwa umezuka hivi punde katika nyumba iliyopo Mtaa wa Jamhuri na Mosque jijini Dar es Salaam na kuteketeza mali mbalimbali.

Taarifa za awali zinaeleza bado chanzo cha moto huo hakijafahamika. Tayari polisi wa zimamoto wamewasili eneo la tukio katika Mtaa wa Jamhuri na Mosque. Pia, askari wa Jeshi la Polisi wamewasili katika eneo la tukio. Eneo la tukio baadhi ya mashuhuda sasa wanaokoa gari moja ambalo lipo karibu na nyumba inayoteketea.

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post