MDIMU: WANAO UNGA MKONO VITA DHIDI YA MAUAJI YA ALBINO MKONO JUU

 Henry Mdimu
"Ni kweli mimi ni Albino, nimejikubali na nimeishi maisha yangu yote bila kujali nilivyo. Sijawahi kutumia hali yangu kupata kitu kwa huruma, nimeyapigania maisha yangu na nimepiga hatua.

Leo hii naongea nanyi nikiwa Baba, Mume, Mwandishi Mwandamizi, Blogger, na mengine mengi, lakini hali yangu sasa inaanza kunikwaza.

Haya mauaji jamani, nimejiteua kuwa Balozi, nitatetea, na kusimama mbele ya wenzangu wote wenye hali kama hii, kama ni wanasiasa ama wafanyabiashara, wanataka kutuua kwa maslahi binafsi, mwaka huu HAPANA.

Wanaoniunga mkono mikono juu"
Mwisho wa kunukuu.

Nikiwa kama Blogger na Mwanahabari, Henry Mdimu aliejitolea kuwa Balozi, nanyoosha mkono juu kwa kuunga mkono kupiga vita vikali mauaji ya ndugu zetu wenye Albinism. kwani wao pia ni Binadamu kama tulivyo mimi na wewe.

LINDIYETU BLOG NA UONGOZI WAKE WOTE UKIONGOZWA NA ABDUL AZIZ UMENYANYUA MIKONO JUU KUUNGANA NAWE ZEE LA NYETI.

JAMANI SASA BASI, NA KILA MMOJA WETU AWE MLINZI KWA NDUGU ZETU HAO.

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post