AUNTY EZIKIEL:: MWANANGU ATANIFUTA MACHOZI YA KUFIWA

Aunty Ezekiel.Mkali wa filamu Bongo, Aunty Ezekiel.

MKALI wa filamu Bongo, Aunty Ezekiel amefunguka kuwa pamoja na kupoteza wazazi wake miaka kadhaa nyuma pindi akiwa mdogo, anaamini mtoto atakayejifungua atamfuta machozi ya muda mrefu ya kuwapoteza wazazi wake.
Aunty Ezekiel.
Aunty alifunguka ishu hiyo kwa upole, ambapo alisema kifo cha wazazi wake kilimfanya kulelewa na bibi yake pamoja na shangazi.
“Kutokuwa na wazazi ni pigo kubwa kwangu, lakini hata hivyo naamini kwamba mwanangu atakuwa na furaha ambayo nilikuwa naipata kutoka kwa wazazi wangu, atakuwa ni zaidi ya rafiki au ndugu, ndiye atakayenifuta machozi ya kufiwa,” alisema Aunty.

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post