Unknown Unknown Author
Title: UKATILI TANZANIA:: AUWAWA KWA SHOKA, ANYOFOLEWA ULIMI
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
IMANI ya ushirikina, ajali na vitendo vya ukatili dhidi ya binadamu vimesababisha wananchi wa mikoa ya Mbeya kugubikwa na simanzi kuto...

Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani Mbeya Barakael Masaki

IMANI ya ushirikina, ajali na vitendo vya ukatili dhidi ya binadamu vimesababisha wananchi wa mikoa ya Mbeya kugubikwa na simanzi kutokana na mauaji ya kutisha.

Imeripotiwa kuwa watu watatu wamefariki dunia mkoani hapa katika matukio tofauti yakiwemo mawili ya mauaji ya kinyama.
Miongoni mwa matukio ya mauaji hayo ni pamoja na la mkazi wa kijiji cha Mkutano wilayani Momba, Hamis Simwawa (25) aliyekutwa shambani akiwa ameuawa kwa kukatwa shoka shingoni na kisha kunyofolewa viungo vya mwili ikiwemo ulimi, meno ya chini na jicho la kushoto.

Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani Mbeya Barakael Masaki alisema mwili wa Hamis ulikutwa Januari 26 mwaka huu majira ya saa mbili asubuhi katika kijiji cha Mkutano kilichopo katika kata ya Nzoka wilayani Momba.

Kaimu Kamanda Masaki alisema kabla ya mauaji kijana huyo aliitwa kwenda kusaidia shughuli za shamba na alipofika shambani ndipo walimuua kwa kumkata na shoka shingoni kabla ya kumnyofoa ulimi, meno ya chini na jicho la kushoto na kupeleka viungo hivyo kusikojulikana.

Alisema tukio hilo linahusishwa na imani za kishirikina ambapo Kawawa Sinkala (31) na Emmanuel Sinkala (15) wakazi wa kijiji cha Mkutano wanashikiliwa na polisi kuhusiana na mauaji hayo.

Katika tukio la pili, Kaimu Kamanda Masaki alisema Mwinzala Sekele mwenye umri wa kati ya miaka 40 na 45 mkazi wa kitongoji cha Chang’ombe kilichopo kijijini Mshewe wilayani Mbeya aliuawa kwa kupigwa sehemu mbalimbali za mwili wake na kundi la wananchi walioamua kujichukulia sheria mkononi.

Alisema mwili wa marehemu ulikutwa Januari saa kumi na moja alfajiri ukiwa umetelekezwa kijijini mshewe kata ya Bonde la Usongwe wilayani Mbeya.

Kwa mujibu wa Kaimu Kamanda Masaki inadaiwa kuwa chanzo cha mauaji hayo ni kulipiza kisasi kufuatia Sekele kutuhumiwa kuhusika na mauaji yaliyotokea awali Januari 24 mwaka huu majira ya saa tisa alasiri ambapo mkazi wa kijiji cha Mshewe Sekela Kaini alikutwa ameuawa na mwili wake kutupwa kwenye shamba la mahindi kijijini hapo.

Katika tukio lingine mkazi wa Ilomba jijini Mbeya Joshua Mwaisanila (35) alifariki dunia baada ya kugongwa na lori lenye namba T 189 BLKs Semi Trailler lililokuwa na tela lenye namba T 193 BLK lililokuwa likiendeshwa na Ahazi Cheyo (24) mkazi wa Iyunga jijini Mbeya.
Kaimu Kamanda Masaki alisema ajali hiyo ilitokea Januari 26 mwaka huu saa tatu asubuhi maeneo ya Forest barabara kuu ya Mbeya/ Tunduma na dereva wa lori hilo anashikiliwa na polisi wakati chanzo cha ajali kinachunguzwa.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top