Unknown Unknown Author
Title: SIRI YA KASI YA USAIN BOLT YAFICHULIWA
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Wanasayansi wanasema kwamba wanaweza kueleza kasi ya mwanariadha maarufu sana duniani Usain Bolt inatokana na nini kwa kutumia hisabati au...
Wanasayansi wanasema kwamba wanaweza kueleza kasi ya mwanariadha maarufu sana duniani Usain Bolt inatokana na nini kwa kutumia hisabati au hesabu.
Usain Bolt
Bolt alivunja rekodi kwa kumaliza mbio za mitya 100 kwa sekunde 9.58 wakati wa mashindano ya kimataifa mwaka 2009 mjini Berlin. Na hio ndio rekodi ya dunia.

Wanasayansi hao wanasema utafiti wao unafafanua kwamba nguvu na uwezo wa kimeili wa Bolt kuweza kustahimili upepo unasaidiwa na urefu wake wa futi 6 inchi 5.

Hata hivyo wanasanaysi hao wanasema bado wanafanya uchunguzi kujua kinachowafanya wanariadha wazuri kukimbia kwa kasi.

Kulingana na utafiti wa wanasayansi hao waliotumia hesabu, kasi ya Bolt ya sekunde 9.58 mjini Berlin iliwezekana baada ya mwanariadha huyo kukimbia mita 12.2 kwa sekunde sawa na kasi ya mita 27 kwa saa. .

Walisema kuwa Bolt alipata nguvu zake pindi alipoanza kukimbia chini ya sekunde moja na hiyo ilikuwa nusu tu ya kasi yake yote.

Wanafizikia hao wanasema hii ina maanisha kuwa hapo ndipo hewa hupunguza nguvu zake za kusongesha vitu.

Pia waligundua kwamba chini ya asilimia nane ya nguvu za misuli yake ilitumika wakati alipokuwa anakimbia,

Rekodi ya Bolt mjini Berlin, ilikuwa nzuri zaidi kushuhudiwa tangu kuanza kutumika kwa kifaa cha elektroniki kuhesabu saa mwaka 1968.

''Ni vigumu sana kuvunja rekodi siku hizi, hata kwa sekunde moja kwani wanariadha wanahitajika kutumia nguvu nyingi sana dhidi ya upepo ambao huongezeka kwa kila ongezeko la kasi, '' walisema wanafizikia walofanya utafiti huo.

John Barrow wa chuo kiuu cha Cambridge alisema kwamba kasi ya Bolt pia ilitokana na ukubwa wa hatua zake za miguu licha ya kuanza mbio kwa kuchelewa.

"misuli yake inamsaidia sana kuongeza kasi licha ya kwamba mwenyewe ana kasi ya juu.''

Wanasema kwamba Bolt ana uwezo mkubwa wa kuvunja rekodi zaidi ikiwa ataanza mbio zake haraka na kwa kasi ikilinganishwa na mtindo wake wa sasa.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top