ALICHOKISEMA CRISTIANO RONALDO DHIDI YA MCHEZAJI MWENZAKE WA REAL MADRID GARETH BALE HICHI HAPA

Mwanasoka bora wa dunia kwa mwaka 2014, Cristiano Ronaldo dos Santos Aveiro, amewataka mashabiki wa klabu ya Real Madrid kumuonyesha ushirikiano wa kutosha mshambuliaji wa pembeni kutoka nchini Wales Gareth Frank Bale.

Ronaldo, ametoa wito huo kwa mashabiki wa Real Madrid kwa kuamini Bale bado ana nafasi ya kuendelea kufanya vyema na kufikia hatua ya kuwa mchezaji bora duniani.

Ronaldo amesema Bale tangu alipojiunga na Real Madrid amekua na mchango mkubwa katika kikosi cha The Meringues ambacho kwa mwaka 2014 kilitwaa mataji manne.

Amesema anakumbuka hata yeye aliposajiliwa klabuni hapo mashabiki walionyesha kumkubali na kuendelea kumpa ushirikiano mpaka amefikia hatua ya kuwa mchezaji bora wa dunia, hivyo anaamini nguvu hizo zikielekezwa kwa Bale mambo yatakua mazuri zaidi siku za usoni.


BOFYA PLAY::

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post