Unknown Unknown Author
Title: KOPUNOVIC ANENA: "NILIJUA SHUJAA WETU ATAKUA IVO MAPUNDA"
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Kocha mkuu wa klabu ya Simba, Kopunovic, amesema kuwa kutokana na uzoefu alionao katika mchezo wa mpira wa miguu hasa akiwa langoni kipa ...
Mabingwa wa Mapinduzi Cup 2015 Simba
Kocha mkuu wa klabu ya Simba, Kopunovic, amesema kuwa kutokana na uzoefu alionao katika mchezo wa mpira wa miguu hasa akiwa langoni kipa namba moja wa timu hiyo Ivo Mapunda, Alijua kuwa atawasaidia katika kuokoa mikwaju ya penati kwenye mchezo wa fainali uliopigwa jana usiku na Simba kuibuka na ushindi wa penati 4-3 dhidi ya Mtibwa.

Kopunovic amesema hayo jana usiku baada ya mchezo huo kumalika katika Uwanja wa Amani hapa visiwani Zanzibar, ambapo mabingwa hao wa michuano ya tisa ya kombe la mapinduzi walikabidhiwa kikombe chao na Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dr. Ally Mohamed Shein.

“Niliamua kumtoa Manyika na kumuingiza Ivo nikijua kabisa huyu ni mkongwe, na anauwezo mkubwa wa kudaka penati, kwahiyo ubingwa huu yeye ndio ameuleta kwani amepangua penati muhimu sana iliyotupatia kombe” Amesema Kopunovic.

Mabingwa wa Mapinduzi Cup 2015 Simba
IVO NA KOCHA WAKE WAKISHANGILIA USHINDI

Kocha huyo jana alifanya mabadiriko ya kumtoa aliyekuwa kipa wa michuano hiyo toka inaanza Peter Manyika na kumuingiza Ivo Mapunda ambaye hakuwepo toka mwanzo kufatia kuwa katika 40 ya Mama yake, ingawa alirudi na kujiunga na timu katika mchezo wa nusu fainali lakini hakucheza hadi hapo jana ambapo aliibeba Simba katika mikwaju ya penati.

Ubingwa huo unakuwa wa kwanza kwa kocha huyo ambaye bado hajamaliza mwezi akiwa na Simba baada ya kuchukua mikoba ya aliyekuwa kocha wa Simba Mzambia Patrick Phiri ambaye alitimuliwa kufatia matokeo mabaya ya sare.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top