Unknown Unknown Author
Title: AFYA:: MAUMIVU MAKALI WAKATI WA TENDO LA NDOA NA MADHARA PAMOJA NA UFUMBUZI WA TATIZO
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Maumivu wakati wa tendo la ndoa au kuumia wakati mnafanya tendo la ndoa kwa mwanamke hujulikana kama Dyspareunia. Neno Dyspareunia tamka...
Maumivu wakati wa tendo la ndoa au kuumia wakati mnafanya tendo la ndoa kwa mwanamke hujulikana kama Dyspareunia.
Maumivu
Neno Dyspareunia tamka (dis-pa-roon-ia) linatokana na neno la kigiriki lenye maana ya shida katika kuingiliana wakati wa kufanya tendo la ndoa (difficulty mating au badly mated).

Utafiti unaonesha kwamba kati ya wanawake watatu, wawili wamewahi au hupata maumivu wakati wa tendo la ndoa.

Imefika kwamba baadhi ya ndoa, mwanamke anapata maumivu kiasi cha kutokuwa na hamu tena ya tendo la ndoa na matokeo yake wamekuwa na wakati mgumu linapokuja suala la kufanya mapenzi na pia kila wakirudia kufanya tendo la ndoa, mambo ni yamekuwa ni yaleyale kwa mwanamke kuumia zaidi kuliko mara ya kwanza.

Kawaida huwa haifurahishi kabisa na haina hata ladha kufanya tendo la ndoa huku mmoja kati yenu akiwa anapata maumivu makali au shida hiyo husababisha kutojishughulisha katika kuleta raha ya kweli na hatimaye kuridhishana kimapenzi wakati wa tendo la ndoa.

Tendo la ndoa halikuwekwa ili kukupa shida au maumivu bali kukupa raha, furaha na kuridhishwa.
Moja ya kanuni muhimu sana katika tendo la ndoa ni
“ Kama unapata maumivu usifanye”
Badala yake tafuta nini kimesababisha na tafuta jibu sahihi la kuondoa hiyo hali au muone daktari akusaidie.

Na baada ya kupata tiba na kupona ndiyo unaruhusiwa kuendelea kufanya tendo la ndoa kwa kufurahia na kukupa raha zaidi, vinginevyo itakuwa ni kuleta maangamizi.

Ni kweli kwamba kama moja wapo ya mahitaji ya msingi ya kihisia (emotions) kama hili la tendo la ndoa halipatikani katika ndoa linaweza kusababisha mmoja ya wanandoa kutokuwa mwaminifu kwa mwenzake na kutoka nje kwenda kutafuta mtu wa kumridhisha zaidi, hata hivyo kwa mwanamke kufanya tendo la ndoa huku anapata maumivu au kuumia kwa kuogopa kwamba asipompa Mume wake haki yake basi anaweza kutoka nje na kutokuwa mwaminifu hilo si sahihi kwani ni kutojiamini na kutojali si afya yako tu bali haki yako ya msingi ya kufanya tendo la ndoa kwa kupata raha.

Mnahitaji kujulishana na kuelezana ukweli ili muweze kupata dawa na hatimaye kurudi kwenye raha upya badala ya kuumizana.

Kuna mambo mengi yanayosababisha mwanamke au hata mwanaume kupata maumivu wakati wa tendo la ndoa na inaweza kuwa ni wakati mwanaume anapoingia (penetrate) au wakati wa kitendo chenyewe au baada ya kitendo chenyewe. 

Inaweza kuwa ni maumivu makali sana au inaweza kuwa ni kuwashwa au inaweza kuwa ni maumivu wakati wa kukojoa mkojo wa kawaida au inaweza kuwa ni maumivu ambayo unasikia kama moto unawaka vile ndani yako wakati wa tendo la ndoa.

Sababu zinazosababisha Maumivu wakati wa tendo la ndoa kwa mwanamke;-
a)Fibroids; uvimbe katika kizazi unaowatesa wanawake Tanzania
KATIKA siku za hivi karibuni, wanawake nchini wamekuwa wakilalamika kuwa kila wanapokwenda kujifungua basi hukutwa na uvimbe katika nyumba ya uzazi.
Uvimbe huo, ambao si saratani, umekuwa ni tishio kwa maelfu ya wanawake nchini jambo linalosababisha wengi wao kuondolewa vizazi vyao.

wanaPatholojia wanaulezea ugonjwa huu kuwa ni fibroids kwa kitaalamu ‘leimyoma’ ni uvimbe unaowapata asilimia 25 ya wanawake wa Kiafrika na asilimia 50 ya Wazungu.
Uvimbe huu si saratani, unajitokeza ama katika ukuta wa kati, wa nje au ndani kabisa ya nyumba ya uzazi,” 

Pia uvimbe huu huwa katika umbile la misuli myembamba na laini na hukua siku hadi siku,sababu kuu ya ugonjwa huu, bado haijajulikana. pamoja na kuwa sababu kuu haijajulikana, lakini zipo sababu ambazo zimehakikiwa kusababisha mwanamke kupata uvimbe wa fibroids.Sababu inayopewa kipaumbele zaidi ni wingi wa vichocheo vya ‘estrogen’ ambavyo vipo katika miili ya wanawake,vichocheo hivi ndivyo hufanya kazi katika mwili wa mwanamke na kumsababishia kupata siku zake za hedhi. 
“Ndiyo maana wengi wanaopata uvimbe huu, huwa ni wanawake walio katika balehe au ambao tayari wamevunja ungo, kwani ndiyo ambao huzalisha vichocheo vya estrogen,Lakini, pia endapo inatokea mwanamke akapata matibabu ambayo yatamtaka kuongezewe vichocheo hivi, huwa katika hatari ya kupata uvimbe huu. ndiyo maana wanawake walio katika kikomo cha hedhi(menopause) na watoto hawawezi kupata uvimbe huu. 

Sifa kuu za ugonjwa huu , huwa ni nyingi kwa sababu ni uvimbe ambao asili yake ni mishipa midogo midogo na inapokuwa huweza kufikia urefu wa sentimeta tano na zaidi na uzito wa kilogram 10.Uvimbe huu unaweza kutokea katika kuta zote za kizazi cha mwanamke na kusababisha mwanamke ang’olewe kizazi chake. “Hata hivyo, wanawake wengi hupata uvimbe huu katika ukuta wa ndani kabisa wa kizazi,
Sifa nyingine za uvimbe huu ni kuwa na tabia yake ya kubadilikabadilika sana.Kwa mfano, fibroids huweza kubadilika rangi na kuwa ya njano, ikabadilika na kuwa katika hali ya kimiminika, baadaye kuwa ngumu au kuwa laini yenye kutomasika.

Dalili za Fibroids
Ni vigumu mwanamke kubaini au kuhisi dalili zake.“Dalili hutegemeana na eneo ulipokaa uvimbe na ukubwa, wengi hugundulika wakati wa kujifungua, na ujauzito au endapo mwanamke atapata uvimbe katikati ya kizazi, basi huweza kutokwa damu kwa wingi,Hata hivyo, asilimia 35 hadi 50 ya wanawake wanaougua maradhi haya huonyesha dalili wakati wa kujifungua,.
Dalili nyingine ni mwanamke kutokwa damu zake za hedhi kwa wingi na kwa siku nyingi. Damu za hedhi huweza kuwa nyingi au kidogo sana zikiambatana na maumivu makali. Asilimia 30 ya wanawake wanaopata maumivu na damu nyingi wakati wa hedhi huwa na uvimbe wa aina hii.Wakati mwingine mwanamke huweza kuhisi ana ujauzito kwani uvimbe huu huwa mkubwa na huchezacheza kana kwamba ni kiumbe.

Nina mifano hai, wapo wanawake waliowahi kuhisi wana ujauzito, wakakosa kabisa siku zao za hedhi, wakapata dalili zote za ujauzito na kumbe walikuwa na uvimbe wa fibroids,mara nyingi uvimbe unaojitokeza katika ukuta wa nje wa kizazi na kuning’nia, ndiyo hucheza na kuleta dalili za ujauzito.Mwanamke huweza kuvimba miguu kwa sababu uvimbe huu husababisha damu isitembee.

Dalili nyingine kuwa ni mwanamke kupata maumivu wakati wa tendo la ndoa.Wakati mwingine, fibroids hukua na kuzuia mfumo wa mmeng’enyo wa chakula na kusababisha mwanamke avimbiwe. Vile vile, uvimbe huo huweza kuzuia kibofu cha mkojo, na kumfanya mwanamke apate haja ndogo kwa taabu , au akatokwa na uchafu ukeni.

Hatari kuu ya uvimbe huu ni ugumba, asilimia 27 hadi 40 ya wanawake wanaopata uvimbe katika kuta zote za kizazi, hushindwa kupata watoto.
Hatari nyingine ni kwa wanawake wajawazito wenye uvimbe huu ambao wengi hufanyiwa upasuaji kwani fibroids huweza kuzuia mlango wa kizazi na mwanamke kushindwa kujifungua. Imebainishwa kuwa, asilimia 30 ya wanawake hutolewa vizazi mara baada ya kujifungua kutokana na uvimbe huu.

Tahadhari, wanawake walio katika umri wa kuzaa lakini hawazai wapo katika hatari ya kupata maradhi haya. Hii ni kwa sababu vichocheo vya estrogen hukua kwa wingi na kusababisha misuli ya fibroids kukua, lakini vichocheo hivyo huacha kukua wakati wa ujauzito,

Walio katika hatari hii ni watawa ambao hawatakiwi kuzaa au wale wanaopitiliza umri wa kuzaa.
Watalaamu mbalimbali wa afya ya uzazi wanashauri wanawake kwenda kufanyiwa uchunguzi mara kwa mara ili kubaini maradhi ambayo mengine yanaweza kutibika au kuzuilika

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top