Unknown Unknown Author
Title: WANANCHI WATAKIWA KUCHUNGUZA NA NAKUHOJI SABABU ZA ONGEZEKO LA MAPATO YATOKANAYO NA MAZAO YA MISITU.
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Wadau wa mazao ya misitu waliohudhuria warsha ya wadau wa Mjumita iliyofanyika Dodoma Bi Sophia Masuka afisa mawasiliano wa Mama misitu ...
Mjumita Wadau wa mazao ya misitu waliohudhuria warsha ya wadau wa Mjumita iliyofanyika Dodoma
Mjumita Bi Sophia Masuka afisa mawasiliano wa Mama misitu akitoa elimu juu ya mradi wa Mama Misitu kwa wadau waliofika katika warsha hiyo
Mjumita Wadau wa mazao ya Misitu wa wilaya ya Kilwa wakibainisha baadhi ya changamoto wanazokutana nazo katika biashara ya Mkaa, Mbao na Magogo katika kikao kilichoitishwa na Jumuiko la maliasili Nchini (TNRF) Baada ya kumalizika kwa warsha ya wadau wa shirika la mpingo wilayani kilwa

Na.Abdulaziz Video, Dodoma
Jamii imetakiwa kuchunguza na kuhoji sababu za ongezeko la mapato yanayotokana na mauzo ya bidhaa za misitu badala ya kushangilia ili kujiridhisha kama mapato hayo yanatokana na vyanzo halali pasi.

Wito huo umetolewa na meneja wa kampeni ya mama misitu inayoendeshwa na jumuiko la maliasiliTanzania (TNRF), Bw Gwamaka Mwakyanjala alipozungumza na washiriki wa warsha ya mtandao wa jumuia wa usimamizi wa misitu Tanzania (MJUMITA) pamoja na wadau wa shirika la kuhifadhi na kuendeleza Mpingo ambapo alibainisha kuwa jamii ina wajibu mkubwa wa kuchunguza na kuhoji ongezeko la mapato yanayotokana na mazao ya misitu badala ya kufurahia takwimu za ongezeko la mapato hayo inayotolewa nwakala wa Misitu Nchini ili kubaini vyanzo na njia zilizotumika kukusanya mapato hayo bila ya kuathiri Misitu

Gwamaka alibainisha jkuwa mapato yanayotokana na faini wanazotozwa wavunaji haramu na wasiozingatia sheria,taratibu na kanuni za uvunaji na hivyo kusababisha kuongezeka mapato wakati misitu ikiwa inaendelea kuteketea

“wananchi wana haki ya kushiriki moja kwa moja katika kusimamia na kuhakikisha taratibu zinafuatwa kuanzia hatua ya kuvuna,kuchakata na kuuza mazao ya misitu ili kuepuka udanganyifu unaosababisha uharibifu wa misitu na mazingira".

"mnaweza kusikia au kuambiwa kwamba mapato yanayotokana na mazao ya misitu yameongezeka kwa kukusanya mabilioni ya fedha,msitosheke na maelezo hayo bali TAFUTENI na mjiridhishe ili kuepuka udanganyifu utakaosababisha kuharibu na kumaliza misitu yenu." alimalizia Gwamaka.

Katika warsha hizo za wadau wa Misitu zilizo chini ya Shirika la Mpingo wilayani Kilwa pamoja na Mtandao wa Jumuiya za Usimamizi wa Misitu Tanzania (MJUMITA) zilizofanyika Dodoma na Kilwa Jumuiko la Maliasili Nchini (TNRF) Liliwezesha wanamtandao toka wilaya ya Mkinga na Kilwa pamoja na wanahabari kuhudhuria warsha hizo ili kubaini baadhi ya changamoto za Misitu ikiwa pamoja na kupata elimu dhidi ya Biashara ya Misitu ikiwemo kufuata taratibu za kisheria katika biashara ya mkaa,Mbao pamoja na Magogo

Mjumita ..Meneja wa Mradi wa Mama Misitu ,Gwamaka mwakanjala akitoa elimu juu ya matumizi bora ya mazao ya Misitu pamoja na jinsi ya kufanya biashara hiyo kwa mujibu wa sheria
Mjumita Wadau mbalimbali waliohudhuria warsha ya wadau wa jumita iliyofanyika juzi Dodoma
Mjumita
Wanamtandao kutoka wilaya ya Mkinga, Mkoani Tanga waliowezeshwa na TNRF (kupitia program ya ubia na WWF-CEAI inayohusu uwekezaji katika misitu) ndio Ambayo iliwezesha wanavijiji wa vikundi pamoja na waandishi wa habari

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top