Unknown Unknown Author
Title: ROSE NDAUKA AAMUA KUFUNGUKA JUU YA MTU ANEYEMPA MAPENZI YA DHATI KWA SASA
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
HATIMAYE diva wa filamu Bongo, Rose Ndauka ametoa kali ya mwaka kwa kudai kuwa baada ya kutengana na mzazi mwezake sasa hapati tabu tena ...
HATIMAYE diva wa filamu Bongo, Rose Ndauka ametoa kali ya mwaka kwa kudai kuwa baada ya kutengana na mzazi mwezake sasa hapati tabu tena kwani mama yake mzazi amechukua nafasi hiyo na anampa mapenzi ya dhati ambayo hajawahi kupewa na mwanaume yeyote.
Rose Ndauka.
Diva wa filamu Bongo, Rose Ndauka.
Akizungumza na Uwazi, Rose alisema pamoja na kuwa kwenye uhusiano kwa muda mrefu lakini hakuwahi kupata mapenzi ambayo sasa anapewa na mama yake pamoja na mtoto wake ambao mara zote wamekuwa pamoja.“Mama na mtoto wangu ndiyo wanaonipa mapenzi ya dhati hakuna wengine, mwanaume hafiki kwenye upendo wa mama, sasa hivi najisikia kuwa huru sana kwa sababu kile nachokihitaji huwa nakipata kwa mama,” alisema Rose. Rose alikuwa akiishi na mchumba wake, Malick Bandawe ambapo waliachana, Septemba mwaka huu.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top