PICHA ZA IRENE UWOYA KATIKA JARIDA LA VIBE, NI SHEEDAH...NAYE AME #BRAEKTHEINTERNET

Irene uwoya on vibe magazine
Jarida la maswala ya burudani, liitwalo Vibe Tz lililotoka hivi karibuni, limepambwa kwa picha za muigizaji wa filamu hapa Bongo, Irene Uwoya ambaye ni mrembo aliyebarikiwa sura na umbo matata bila kusahau rangi yake, kitu ambacho huwafanya vidume wengi kupagawa na kuwa na mashabiki wengi wa kazi zake mbali nakipaji chake katika sanaa.

Japokuwa kwasasa ni mama wa mtoto mmoja , Uwoya amefanya kile kinaitwa siku hizi –KU-BREAK THE INTERNET, kwenye picha alizopigwa na jarida hilo.

Irene ametokelezea kwenye kurasa za mbele yani “Cover Pages” akiwa amevalia mavazi ya ufukweni ya rangi nyeusi na nyeupe, moja akiwa anatazama mbele na nyingine akitupa mgongo.

Vivazi hivyo vimefanya sehemu kubwa ya mwili wake kuonekana na watu kuweza kujionea uumbaji wa alieviumba. Pia picha zingine zimeonekana kwenye kurasa za kati za jarida hilo akiwa katikati mapozi tofauti tofauti.

Kama haujafanikiwa kuziona zicheki hapo chini . Kisha sema chochote kuhusu picha hizo.
Irene uwoya on vibe magazine


Irene uwoya on vibe magazine

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post