Meneja wa klabu ya Chelsea Jose Mourinho amekisifia kikosi chake kwa kusema ndio kikosi bora kwa sasa kutokana na mwenendo mzuri alionao na anaamini suala hilo litaendelea kuwapa morari wachezaji wake kucheza kwa kujituma na kuuona kila mchezo kama fainali.
Amesema mpaka sasa kikosi chake kinaongoza msimamo wa ligi ya nchini England, pia kipo katika nafasi ya kwanza kwenye msimamo wa kundi la saba la michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya, na kingine anachojivunia ni kuwa katika hatua ya robo fainali ya michuano ya Capital One Cup na kucheza kwa kipindi cha miezi minne bila kufungwa hatua ambayo anaichukua kama sehemu kubwa ya mfanikio aliyokua amejiwekea tangu mwanzoni mwa msimu huu.
Lakini meneja huyo kutoka nchini Ureno mesisitiza kuwa tayari kupokea matokeo yoyote ambayo yatapatikama tofauti na mafanikio aliyoyapata kwa kipindi hiki cha miezi minne tangu msimu wa soka wa barani Ulaya ulipoanza mwezi August mwaka huu.

Mourinho acha kutuyeyusha
ReplyDelete