Unknown Unknown Author
Title: WAYNE ROONEY AONGEZEKA KATIKA LIST YA MAJERUHI, BLIND APONA, HII HAPA LIST KAMILI
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
WAKATI Nahodha wa Manchester United Wayne Rooney Leo hii atapimwa Goti lake kuthibitisha undani wa maumivu yake na pia atakuwa nje kwa mud...
WAKATI Nahodha wa Manchester United Wayne Rooney Leo hii atapimwa Goti lake kuthibitisha undani wa maumivu yake na pia atakuwa nje kwa muda gani, Klabu hiyo imepata habari njema baada ya Kiungo Daley Blind kupata nafuu na huenda akawa fiti kabisa kabla ya mwisho wa Mwezi huu baada nae kuumia Goti.Wayne RooneyRooney hakucheza Mechi ya Ligi Kuu England Jumanne Usiku Uwanjani Old Trafford wakati Man United inaifunga Stoke City 2-1 baada kuumia Goti Jumamosi iliyopita wakati wanaifunga Hull City.
Meneja wa Man United, Louis van Gaal, amesema: “Rooney atachunguzwa zaidi Goti lake Jumatano. Natumai hakuumia sana.”

Nae Blind alieumia Goti akiichezea Timu ya Taifa ya Netherlands anatarajiwa hivi karibuni kurejea Mazoezini.

Tangu aanze kuifundisha Man United, Van Gaal amekumbwa na Majeruhi wengi na kwenye Mechi na Stoke City Mastaa wake wakubwa kina Angel Di Maria, Luke Shaw na Daley Blind vile vile hawakucheza.
Van Gaal amethibitisha kuwa Rooney na Di Maria hawataweza kucheza Mechi yao ijayo ya Ligi Jumatatu Ugenini na Southampton kwani ni mapema mno kwao.

Hata hivyo, Van Gaal amesema majeruhi wao wengi sasa wanapona na wameanza kurejea Mazoezini.

Manchester United-Listi ya Wachezaji walioumia Msimu huu:

Kipa: David De Gea

Viungo: Angel Di Maria, Juan Mata, Michael Carrick, Daley Blind, Ashley Young, Ander Herrera, Antonio Valencia, Anderson, Marouane Fellaini, Jesse Lingard

Mabeki: Rafael, Luke Shaw, Phil Jones, Marcos Rojo, Jonny Evans, Chris Smalling, Paddy McNair, Tom Thorpe

Mafowadi: Radamel Falcao, Wayne Rooney, Robin van Persie, James Wilson

RATIBA: LIGI KUU ENGLAND **Saa za Bongo, Jumatano Desemba 3

2245 Arsenal v Southampton

2245 Chelsea v Tottenham

2245 Everton v Hull

2245 Sunderland v Man City

Jumamosi Desemba 6

1545 Newcastle v Chelsea

1800 Hull v West Brom

1800 Liverpool v Sunderland

1800 QPR v Burnley

1800 Stoke v Arsenal

1800 Tottenham v Crystal Palace

2030 Man City v Everton

Jumapili Desemba 7

1630 West Ham v Swansea

1900 Aston Villa v Leicester

Jumatatu Desemba 8

2300 Southampton v Man Utd

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top