#FILAMU :: ‘NIMEKUBALI KUOLEWA" YA DR CHENI YARUHUSIWA KUTOKA, KAA MKAO WA KULA

Msanii wa filamu, Mahsein Awadh Said aka Dr. Cheni amesema filamu yake ya ‘Nimekubali Kuolewa’ iliyokuwa imezuiwa kutoka na Bodi ya Filamu Tanzania (TFB) inatarajiwa kutoka mapema mwakani baada kukamilisha matakwa yao.
Nimekubali Kuolewa ya Dr Cheni
Dokta Cheni alisema kuzuiliwa kwa filamu hiyo kulimnyima raha kiasi cha kumfanya asifanye kazi nyingine mpaka akamilishe kazi hiyo.

“Nimefanikiwa kuipigania filamu yangu ya ‘Nimekubali Kuolewa’, itatoka mwezi wa pili mwakani. Kikubwa nilichokifanya ni kurekebisha baadhi ya vitu ambavyo walihitaji na imekamilika kwahiyo watu wakae mkao wa kula tu,” alisema Cheni.

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post