Unknown Unknown Author
Title: MAMA ATUPA KICHANGA CHAKE CHA SIKU MOJA, RONDO MKOANI LINDI
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Kamanda wa polisi Mkoa wa Lindi Renata Mzinga Kamanda wa Polisi amesema mtoto huyo mchanga  amekufa Septemba 17 mwaka huu, baada ya k...
Kamanda wa polisi Mkoa wa lindi renata mzinga
Kamanda wa polisi Mkoa wa Lindi Renata Mzinga

Kamanda wa Polisi amesema mtoto huyo mchanga amekufa Septemba 17 mwaka huu, baada ya kutupwa kichakani na mama yake mzazi aitwae Fatu Mohamedi (35) mkazi wa kijiji cha Ruponda, Kata ya Rondo, wilaya na mkoa wa Lindi.

"Taarifa ya kutupwa kwa kichanga huyu zimepatikana kupitia kwa mtendaji wa kata hiyo, Msafiri Wanie, baada ya kupewa taarifa kuwa mwanamke huyo amemtupa kitoto chake chenye umri wa siku moja"Alisema Mzinga.

Mzinga amewaambia waandishi kuwa baada ya kuokotwa kwa mtoto huyo na kufanyiwa uchunguzi na Daktari wa kituo cha Afya kata ya Rondo alibainika alikuwa tayari ameshakufa.

Amesema tayari mwanamke huyo anashikiliwa na Polisi na katika mahojiano amesema alichukuwa uwamuzi wa kumtupa kichanga chake kutokana ugumu wa maisha, ikiwemo mwanaume aliyezaa naye kukataa kumsaidia katika matunzo yake.

Kamanda huyo wa Polisi mkoani Lindi, amesema mtuhumiwa huyo atafikishwa mahakamani mara baada ya kukamilisha upelelezi na taratibu za kiofisi, kujibu shitaka linalomkabiri la mauaji.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top