Unknown Unknown Author
Title: HABARI KAMILI, TAHADHARI PICHA ZINATISHA:: ALIYEUWA NAYE AUWAWA KWA KUCHOMWA MOTO HUKO LIWALE MKOANI LINDI
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Mtu mmoja alietambuliwa kwa Jina La Issa Mfaume ameuawa na baadae  kuchomwa moto hadi kuteketea na wananchi wenye hasira kali kufuatia  ...
Mauaji liwale
Mtu mmoja alietambuliwa kwa Jina La Issa Mfaume ameuawa na baadae kuchomwa moto hadi kuteketea na wananchi wenye hasira kali kufuatia mtu huyo kufanya mauaji baada ya kumchoma kisu Marehemu Zalali Ramadhan Lunje ambae alikuwa dereva wa bodaboda na pia ni Baunsa katika ukumbi wa Sanabu Pub iliyopo wilayani Liwale na kutokomea mwishoni mwa wiki.
Kamanda wa polisi mkoa lindi Renatha Mzinga
Kamishna msaidizi ambae pia ni kamanda wa Polisi mkoa wa Lindi, Renatha Mzinga amesema Zalali ameuwawa septemba 19/2014 saa 5:30 usiku, kwa kuchomwa kisu kifuani na mtu aitwae Issa Mfaume, katika ukumbi uitwao Sanabu Pub, uliopo mjini Liwale.

ZALALI, Aliyeuwawa kwa kuchomwa Kisu kifuani

"Huyu marehemu licha ya udereva wa bodaboda pia ni Baunsa Uwa anaelinda kumbi mbalimbali za Starehe, na siku hiyo kulikuwa ukipigwa muziki na yeye alikuwa mlangoni kuangalia tiketi kwa watu wanaoingia ndani"Alisema Mzinga.

Akasema siku hiyo Zalali akiwa mlangoni, Issa Mfaume alifika katika ukumbi huo na kutaka kuingia ndani ya ukumbi bila ya kulipia kiingilio na alipozuiliwa na Baunsa huyo, alichukuwa kisu na kumchoma kifuani, upande wa kushoto na kufariki papo hapo.
mauaji liwale
Mzinga amesema mara baada ya mtuhumiwa kutekeleza unyama huo, alitoweka eneo hilo na kwenda kusikofahamika na Ambapo hii leo alikamatwa na wananchi ambao waliamua Kujichulia sheria na kumpiga hatimae kumteketeza kwa Moto hadi kifo chake.
mauaji liwale
Kufuatia tukio hilo jeshi la polisi linafanya uchunguzi wa kutafuta watuhumiwa walioamua kujichukulia sheria mkononi licha ya marehemu kuwa mtuhumiwa, Alisema Kamanda Mzinga.
mauaji liwale

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top