Unknown Unknown Author
Title: IVO MAPUNDA KUIKOSA YANGA SC OKTOBA 12, ATAKUWA NJE WIKI NANE
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Wakati zikiwa zimebakia takribani wiki mbili kabla ya kukutana na mahasimu wao wa jadi, klabu ya Simba imepata pigo kubwa katika timu. ...
Wakati zikiwa zimebakia takribani wiki mbili kabla ya kukutana na mahasimu wao wa jadi, klabu ya Simba imepata pigo kubwa katika timu.
Ivo mapunda
Kipa namba moja wa timu hiyo, Ivo Philip Mapunda amevunjika kidole mazoezini Zanzibar jana asubuhi na anatakiwa kuwa nje kwa wiki nane- maana yake hataweza kusimama langoni timu hiyo ikimenyana na watani, Yanga SC Oktoba 12.

Daktari wa Simba SC, Yassin Gembe amesema kwamba, Ivo aliumia wakati anachupia mpira katika mazoezi ya asubuhi na kwa bahati mbaya mpira ukamgonga kwenye kidole kidogo cha mwisho mkono wa kulia.

Gembe amesema Ivo alitoka mazoezini baada ya tukio hilo na baadaye akapelekwa hospitali ya Mnazi Mmoja kisiwani humo, ambako baada ya vipimo ikagundulika amevunjika sana. “Si kuvunjika kwa mzaha, amevunjika sana na anatakiwa kupumzika kwa wiki nane, baada ya hapo aanze taratibu, ina maana makadirio ya kurudi tena uwanjani ni hadi baada ya miezi mitatu,”amesema Gembe.

Kuumia kwa Ivo kunatoa nafasi kwa makipa chipukizi, Hussein Sharrif ‘Cassilas’ na Peter Manyika kujibidiisha ili kuziba pengo lake.
Ivo anafanya idadi ya wachezaji wanne tegemeo majeruhi Simba SC, baada ya Paul Kiongera anayetakiwa kuwa nje wiki sita, Haroun Chanongo na Issa Rashid ‘Baba Ubaya’ ambao hawatahitaji zaidi ya wiki moja ya kuwa nje ya Uwanja


********************************************
LindiYetu.com ndio mtandao wako kwa habari za burudani, Siasa, Michezo ya Africa na Nje, Tuwe pamoja huku pia >> Instagram Twitter Na Facebook

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top