Unknown Unknown Author
Title: WAYNE ROONEY AFUNGUKA BAADA YA KICHAPO CHA 5-3, NAKUTOA SALAMU KWA MAADUI WA MANCHESTER UNITED
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Nahodha na mshambuliaji wa klabu Man Utd, Wayne Mark Rooney ameonyesha kuwa na matarajio ya kufanya vizuri msimu huu licha ya kukabiliwa...
Rooney on facebook
Nahodha na mshambuliaji wa klabu Man Utd, Wayne Mark Rooney ameonyesha kuwa na matarajio ya kufanya vizuri msimu huu licha ya kukabiliwa na mwenendo mbovu wa kuanza ligi kuu ya soka nchini Uingereza chini ya meneja kutoka nchini Uholanzi Louis van Gaal.
Rooney, ametoa msisitizo huo kupitia ukurasa wake katika mtandao wa kijamii wa Facebook, ambapo ameandika ana mtazamo tofauti na jinsi ambavyo watu wanavyo wachukulia Man Utd, kutokana na matokeo mabaya ya mwishoni mwa juma lililopita baada ya kufungwa na klabu ya Leicester City mabao 5-3.
Rooney on facebook

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 28, ameongeza kuwa kila anapowangalia wachezaji waliopo kwenye chumba cha kubadilishia nguo, anaona vipaji ambavyo vikichanganywa na umakini wa meneja wao hana shaka kwamba klabu hiyo itapata mafanikio.Man Utd, imekuwa haifanyi vizuri tangu mwanzoni mwa msimu huu na mpaka sasa imeshapoteza michezo miwili, kutoka sare mara mbili na kushinda mmoja

HII NDIO POST YENYEWE::

Post by Wayne Rooney.

********************************************
LindiYetu.com ndio mtandao wako kwa habari za burudani, Siasa, Michezo ya Africa na Nje, Tuwe pamoja huku pia >> Instagram Twitter Na Facebook

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

  1. Cjawapata fresh anamasha kwamba man aiwez kupanda ksa wachezaj uwezo mdogo au hana mashaka anaona inawachezaj wazur na itafanya vyema tu

    ReplyDelete

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top