Unknown Unknown Author
Title: WANANCHI WAMJERUHI KWA MAPANGA MLINZI WA SHAMBA LA DURUBAI KIJIJI CHA MKWAYA LINDI MJINI
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
KAMANDA WWA POLISI MKOA WA LINDI RENATHA MZINGA Na Abdulaziz Lindi Mlinzi wa Shamba la kampuni ya Indo Estates Ltd, lililopo kijiji c...
KAMANDA WWA POLISI MKOA WA LINDI RENATHA MZINGA

Na Abdulaziz Lindi
Mlinzi wa Shamba la kampuni ya Indo Estates Ltd, lililopo kijiji cha Mkwaya, kata ya Mingoyo, Halmashauri ya Manispaa ya Lindi, Abdallah Mussa Pwepweta, amelazwa Hospitalini, baada ya kukatwa mapanga sehemu mbalimbali ya mwili wake, kufuatia vurugu zilizojiotokeza Shambani humo.

Vurugu hizo zimetokana na baadhi ya wakazi wa kijiji hicho, ikiwa ni kulipiza kisasi kitendo cha mwananchi mwenzao, Anthony Laurent Malundi (35) kupigwa risasi na mlinzi wa kampuni hiyo, akidaiwa kuiba korosho kutoka katika Shamba hilo.

Wakizungumza na waandishi Ofisini kwao, baadhi ya watumishi wa kampuni hiyo, Mariamu Abdallah na mlinzi Naziru Haruna Hassani, kwa nyakati tafauti walisema Septemba 19 mwaka huu, saa 7:0 mchana, kundi la vijana wasiopungua (15) walivamia Shamba la kampuni hiyo na kuanza kutikisa na kuokota korosho.

Mariamu Abdallah alisema wakati yeye na watumishi wenzake wakiendelea kuokota na kukusanya korosho kutoka Shambani humo, kundi hilo la vijana liliwasili huku baadhi yao wakipanda juu na kutikisa zao hilo, bila ya kupewa ridhaa kutoka kwa wahusika.

"Tulipoona kundi hilo,tuliwaomba walinzi waje kuwafukuza kwani kutokana na wingi wao sisi peke yetu tusingeweza kuwafukuza"Alisema Mariamu.

Naziru Hassani, mlinzi wa kampuni ya Ulinzi ya Comesha Security Guard ya Mtwara, aliyehusika kumtwanga Anthony Laurence risasi mguu wa kushoto, alisema alipolitaka kundi hilo kuondoka Shambani humo, hawakuwa tayari kutii amri yake, badala yake walimtolea Lugha chafu iliyoambatana matusi na kumrushia mawe.

Alisema baadhi yao wakimrushia mawe,wengine walikuwa wakimfuata eneo alilokuwepo mlinzi huyo, wapo waliokuwa wakipanda juu ya miti hiyo na kutikisa korosho, tendo hivyo ikamlazimu kupiga risasi moja hewani, lakini hawakuonyesha utayari wa kuondoka, huku wakidai ilikuwa ni baruti na siyo risasi halali.

"Kufuatia ubishi wa kutotii amri yangu, nilipiga risasi nyingine iliyokwenda usawa wa mikorosho na kumpata mmoja wao, na kumfikia mwilini mwake na kuanza kukimbia huku na huko"Alisema Mlinzi huyo.

Mlinzi huyo akaeleza kufuatia tukio hilo, kundi hilo la vijana walirejea tena Shambani huku likiwa idadi kubwa ya vijana wakiwa na siraha mbalimbali, yakiwemo Malungu na Mapanga, likiongozwa na mtu aliyetajwa kuwa ni Alfonce Likavara, walijigawa makundi matatu na
kupanga mbinu za kuwazunguka.

Alisema katika mbinu walizozitumia walifanikiwa kuwatia mkononi watumishi wawili akiwemo mwangalizi wa Shamba hilo, waliokuwa wakienda kumsaidia mlinzi huyo, na kuwapora bunduki waliyokuwa nayo huku wakiwashambulia kwa kuwapiga maeneo mbalimbali ya miili yao.

Naziru aliwataja walioporwa bunduki na kupigwa walipokwenda kumsaidia kuwa ni, mlinzi Abdallah Pwepweta na mwangalizi wa Shamba hilo, Abdallah Mussa Mapanga.

"Huyu Pwepweta amekatwa mapanga kichwani,mguuni na mkono wake wa
kulia, wakati Abdallah Mussa Mapanga yeye alipigwa bapa la panga
sehemu mbalimbali ya mwili wake na wote wamekimbizwa Hospitali ya mkoa wa Lindi, Sokoine kwa matibabu"
Alisema Naziru.

Alisema katika vurugu hizo,kundi hilo la vijana lisilopungua (50) limeweza kuondoka na korosho zote zilizokuwa zimekusanywa na kuangushwa kutoka katika Shamba hilo.

Mwandishi wa mtandao huu alifanikiwa kuzungumza na Anthony Laurence Malundi, aliyepigwa risasi mguu wake wa kushoto eneo la pajani, alipokuwa Hospitali ya Sokoine akipatiwa matibabu, na kudai amepigwa risasi hiyo, na mlinzi wa Shamba la kampuni hiyo ya Indo Estates Ltd, alipokuwa akipita njiani kuelekea nyumbani kwake akitokea kwenye Shamba lake.

"Nikiwa napita njiani nikienda nyumbani nikitokea Shambani kwangu, nikasitukia risasi ikitua mguuni mwangu na sikueleza risasi hii napigwa kwa sababu zipi"Alidai Anthony.

Afisa mtendaji wa kijiji hicho, Said Machela, amekiri kutokea vurugu hizo zilizoambatana na milio ya bunduki, zilizosababisha uharibifu wa mali za mashambani na majeruhi ya watu watatu wakiwemo wawili watumishi wa kampuni hiyo.

"Ni kweli vurugu zimetokea Shambani kwa mwekezaji Durubai,huku watu watatu, wakiwemo watumishi wawili na mlinzi mmoja,kuumizwa na kukimbizwa Hospitalini kwa matibabu"Alisema Machela.

Mganga mfawidhi Dkt, Abdallah Mchome, wala mganga mkuu wa Hospitali hiyo, Dkt,Yusufu Sonda, hawakupatikana ili kupata kauli zao, lakini baadhi ya watumishi ambao waliomba kutotajwa majina yao wamethibitisha kupokelewa kwa majeruhi na kupatiwa matibabu, huku mmoja Abdallah Pwepweta akipelekwa Hospitali ya Nyangao iliyopo Lindi vijijini.

"Watu watatu wameletwa hapa, lakini mmoja kutokana na hali yake kuwa mbaya zaidi, amekimbizwa Hospitali ya Nyangao kwa matibabu zaidi"Alisema mmoja wa watumishi hao.

Alisema majeruhi aliyekimbizwa Hospitali hiyo ya Nyangao amekatwa mapanga kichwani, mguuni na mkono wake wa kulia na kubakiza kipande cha nyama pekee kikiwa kinaning'inia.

Kamanda wa Polisi mkoani Lindi, Renatha Mzinga, amethibitisha kutokea vurugu hizo na kueleza wanamshikilia majeruhi wa risasi, Anthony Laurence Malundi, kwa mahojiano zaidi baada ya kuelezwa kuwa ndiye muhusika mkuu wa vurugu hizo, kutokana na kitendo chake cha wizi wa korosho kutoka katika Shamba hilo linalomilikiwa na mwekezaji aitwae
Durubai.

"Ni kweli Mkwaya kumetokea vurugu ikiwemo kujeruhiwa watu akiwemo aliyepigwa risasi na sasa tunamshikilia huyu Anthony kwani tumeelezwa ni mwizi na amepigwa risasi akidaiwa kuiba korosho kutoka katika Shamba hilo"
Alisema Mzinga.

Mzinga amesema moja ya bunduki aina ya Shotigani iliyokuwa imeporwa katika vurugu hizo,imeweza kupatikana pembeni mwa Shamba hilo, huku ikiwa imekatwa kitako chake.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top