ORIGINO KOMEDI YAPATA PIGO

KUNDI maarufu la vichekesho ambalo kwa sasa ni kama halipo, limepata pigo kubwa baada ya aliyekuwa meneja wao, mtangazaji nyota wa zamani wa televisheni, Christina Mosha maarufu kama Seven, kuwamwaga na hivyo kuachana nao.
original comedyBaadhi ya waigizaji wa kipindi cha orijino Komedi kutoka kushoto ni Joti, Wakuvanga, Mpoki, Masanja mkandamizaji na Maclegan.
Akizungumza na gazeti hili juzikati, Seven alisema ameachana nao baada ya mkataba wake wa sasa kumzuia kufanya kazi na watu wengine zaidi ya walio chini ya mwajiri wake mpya.
“Hivi sasa niko na Sony, wao wananizuia kufanya kazi na wasanii ambao hawako nao, hivyo baada ya mkataba wangu na wao kumalizika, nimeamua kuachana nao.
moshaAliyekuwa meneja wa kundi la Ze Comedi, mtangazaji nyota wa zamani wa televisheni, Christina Mosha maarufu kama Seven akifafanua jambo.
Mimi ni mwakilishi wa Sony barani Afrika, ninashughulika na wasanii toka nchi tofauti za Afrika, kama Senegal, Kenya na kwingineko kasoro Afrika Kusini,” alisema.

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post