Wananchi wilayani Kilwa mkoani Lindi wameendelea kunufaika na wawekezaji,baada ya kampuni ya uchimbaji gesi ya PANAFRICAN ENERGY kuikabidhi halmashauri hiyo zahanati ya kijiji cha Nangurukuru ambayo ujenzi wake umegharimu Tshs 262 Milioni .
Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo ambayo yalifuatiwa na utiaji sahihi mkataba wa ujenzi wa nyumba mbili za watumishi wa zahanati hiyo ambazo ujenzi wake hadi kukamilika utagharimu shilingi 458 milioni.
Meneja wa huduma za jamii wa kampuni hiyo, Andrew Kashangaki alisema katika ujenzi wa zahanati hiyo kampuni ya PANAFRICAN ENERGY imechangia jumla ya shilingi 216,000,000 Ambapo pia kutokana na tatizo la wafanyakazi pia kampuni imeamua kufadhili ujenzi wa nyumba mbili za watumishi wa zahanati hiyo ambazo mkataba wenye thamani ya shilingi 458,000,000 ulisainiwa baina ya mkurugenzi mtendaji wa kampuni hiyo Bw David Roberts na Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Kilwa katika hafla hiyo fpi ya kukabidhi zahanati.
Aidha Kashangaki alibainisha kuwa sera ya kampuni hiyo licha ya kufanya kazi ya uzalishaji wa Gesi ya songosongo pia hutoa misaada kwa jamii ikiwemo kufadhili programu ya ufundishaji lugha ya kiingereza kwa wanafunzi wa kidato cha kwanza wa shule za sekondari za halmashauri hiyo, ambapo jumla ya shule za sekondari 20 kati ya 28 zimenufaika na programu hiyo.
"Wana kilwa tulianza kusaidia elimu ya kiingereza kwa kuzifikia shule 20 ila kwa umuhimu wa elimu kuanzia mwakani tutazifikia shule zote 28 za sekondari ikiwemo kusaidia upatikanaji wa Umeme Jua kwa shule ambazo hazina umeme" Alimalizia Kashangaki
"Wananchi wa Kilwa nadhani ni mashahidi kampuni hii imesaidia wilaya yote si Kama Gazeti moja lilivyoandika hivi karibuni Huu ni upotoshaji mkubwa kwani elimu inasaidiwa wilaya yote, Afya Hivyo hivyo, Maji wananufaika mpaka Njinjo na hata mrahaba unaolipwa na kampuni hiyo zaidi ya Nusu inachangia katika sekta ya elimu Tuwe makini kuyajuahaya yenye ukweli si maneno tu ya vijiweni..." Alimalizia Ulega
"Hakika tulishindwa kabisa na Tulifikia hatua ya Kumuomba Rais Kikwete Kusaidia alipokuja katika ziara yake ambapo aliwaagiza Viongozi wa Wilaya kuangalia uwezekano ndipo Mkurugenzi aliehama Bw Mapunda Alifanikisha kuwaomba hawa wahisani na leo wametukamilishia na tunafarijika zaidi walipoamua kutujengea na Nyumba 2 kwa 4 za watumishi itasaidia sana si kwa Nangurukuru tu hata wasafiri watakaopata dharula katika barabara kuu"
Post a Comment Blogger Facebook
Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii
Note: Only a member of this blog may post a comment.