Mwenyekiti wa bodi ya korosho Anna Abdala akifungua kikao cha wadau wa
korosho kilichofanyika wilayani Masasi mkoani Mtwara kulia ni waziri wa
kilimo na ushirika Injinia Christopher Chiza kikao ambacho kimejadili
maendeleo na changamoto za mazao hilo ikiwemo kupanga bei elekezi
2014/2015
BODI zote za mazao nchini zimetakiwa kutatua kero mbalimbali zinazowakabili wakulima ili kuwajengea matumaini ya kuzalisha kwa wingi na kwa viwango vinavyohijtajika kwenye masoko ya ndani na nje na kuliletea taifa fedha za kigeni.
Rai hiyo imetolewa jana wilayani Masasi mkaoni Mtwara na waziri wa kilimo, chakula na ushirika, Injinia Christopher Chiza alipokuwa akifungua mkutano mkuu wa wadau wa korosho Tanzania uliyofanyika wilayani Masasi katika ukumbi wa Emirates mjini hapa.
Alisema bodi zote za mazao hapa nchini zinatakiwa zitatuwe matatizo ambayo wakulima wanakumbananayo na kuwasababishia washindwe kufikia malengo waliyoyakusudia na hali hiyo inatokana na viongozi wa bodi kukwepa kutimiza majukuma yao wanayotakiwa kuyatekeleza.
Chiza alisema kuwa kwa sasa kumekuwa na mwaya mkubwa kati ya bodi,Halmashauri za wilaya na miji,mifuko ya pembejeo na wakulima inayosababishia kutofanya vizuri na kumuacha mkulima akiwa kisiwani bila ya kupata msaada kupitia bodi hizo.
Waziri huyo alisema suala kubwa ambalo linapelekea kuwepo na mwanya huyo kunatokana na kutowashirikisha wakulima kwenye maamuzi mbalimbali ikiwemo kwenye kufanya mahesabu ya uendeshaji yanayohusu manunuzi,gharama za matumizi na malipo ya majaliwa ambayo ni kiini cha mafanikio kwa mkulima.
Alisema kuwa wakulima wa Tanzania wako tayari kuzalisha bizaa za mazao lakini kutokana na viongozi wa bodi zao kushindwa kutekeleza matakwa ya wakulima kwa kutanguliza masilahi yao binafsi badala ya masilahi ya umma yaliyowapeleka madarakani.
"Ili mkulima apewe matumaini ya kuzalisha mazao kwa tija bodi lazima ziwemstari wa mbele katika utendaji wa majukumu yake kwa ufanisi na uaminifu zaidi na kutii sheria ya ushirika na kanuni zake kwakufanya hivi kutamsaidia mkulima,"alisema
Kwa upande wake mwenyekiti wa bodi ya korosho Tanzania, Bi. Anna Abdallah ameiomba serikali kuwaajiri watafiti vijana wenye kada ya utafiti ili kuchukua nafasi zilizoachwa wazi na watafiti wastaafu ambapo vijana watasaidia kuboresha shughuli za utafiti wa kilimo cha
korosho.
Alisema mfano kituo cha utafiti cha Naliendele kilichopo mkoani Mtwara ambapo kwa sasa kituo hicho kimebaki na mtafiti mmoja ambaye hata hivyo yupo kwa mkataba baada ya muda wake wa utumishi kukoma hivyo kufanya zao la korosho kukosa watafiti na kupoteza mwelekeo.
Bi.Abdallah alisema kuwa kumekuwapo na mafanikio makubwa ambapo mwaka 1961-1962 uzalishaji ulikuwa tani 42,000 na mwaka 2011/12 uzalishaji ulipanda kufikia tani 158,714,09 na ongezeko la wilaya zinazolima korosho toka 19 hadi kufikia 43 na mikoa 10 badala ya mitano.
Post a Comment Blogger Facebook
Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii
Note: Only a member of this blog may post a comment.