
Msikiti wa Mtambani ulioko maeneo ya Kinondoni jijini Dar es salaam unawaka moto hivi sasa kama inavyoonekana katika picha na juhudi za kuuzima zinaendelea. Chanzo cha moto huo pamoja na madhara yake bado havijajulikana. Kikosi kazi cha Globu ya Jamii kipo eneo la tukio na tutawapasha habari zaidi baadaye.
Tags
HABARI ZA KITAIFA