Khadija Kaudunde akikabidhiwa zawadi ya Godoro na Mgeni rasmi wa shindno hilo Mkuu wa wilaya ya Kilwa, Abdallah Ulega.
Mshindi wa kwanza wa kusoma Juzuu 30, Abdallah Yusus Kombo, Akipokea zawadi yake ya Baiskeli aliyokabidhiwa na Mgeni Rasmi Mkuu wa wilaya ya Kilwa, Abdallah Ulega.
Viongozi wa Dini wilayani Kilwa mkoani Lindi wametakiwa kuhubiri Amani, umoja na mshikamano wanapokuwapo kwenye ibada zao ili kuliombea Taifa lisiingie kwenye vurugu zinazoweza kusababisha uvunjivu wa amani ya nchi Hususan katika mchakato wa katiba mpya.
Akihutubia waislam walioshiriki katika shindano la kila mwaka la Usomaji wa Quran, Mkuu wa wilaya ya kilwa, Abdallah Ulega ameeleza kuwa viongozi wa dini wana nafasi kubwa katika Kuelimisha na kukemea waumini wao kufanya mambo ambayo yanaweza kusababisha kuleta madhara ya kuwagawa watanzania.
Aidha alibainisha kuwa nchi yetu kwa sasa iko katika kipindi cha mpito cha kutafuta katiba ambapo alitumia nafasi hiyo kutoa wito kwa waislam kukemea tabia za Rushwa, Wizi, Zinaa, Uharibifu wa Mazingira na inawezekana ikiwa Quran itasomwa na kuhifadhiwa kuzingatiwa Ipasavyo.
"Hakika nyie ni mashuhuda Mwezi huu wa Ramadhan hali ni ya Utulivu sana katika mji wetu hakuna Disco, Rusha Roho pamoja na mikusanyiko katika mabar Tena Hata kimavazi watu wanavaa mavazi ya Heshima hali imekuwa ya Amani sana Naomba waislamu wenzagu msiache Tumche Mola wetu"Alimalizia UlegaKwa upande wake kaimu Shekhe mkuu wa wilaya za Kilwa, Sheikh Muhidin Matuta alisema kuwa ni wajibu wa waislamu kujenga upendo baina yao na pamoja na kufundisha maadili kwa watoto ili wawe viongozi bora wa baadaye.
Aidha Sheikh Muhidin alieleza kuwa shindano hilo linaloratibiwa na kamati ya kusimamia Mashindano ya Quran Kilwa(QUROU) licha ya usimamizi huo tayari inamiliki Ardhi ambayo imekusudiwa kujengwa kwa shule itakayowalea na kuwasomesha Mahafidh wa Quran na vinozi jana wengine waweze kuwa miongoni mwa Jamii na Viongozi bora wa Taifa.
"Waislamu wenzangu tupo katika mfungo wa Ramadhan,Mwezi ambao utukufu wake kila mmoja anaujua na jitahada zinafanywa na masheikh na waalimu wa Dini kukumbusha na kuelimisha Faida zinazopatikana katika Mwezi huu hivyo usiaharibu wema wote kwa kufurahia sikukuu ya IDD"Alimalizia kaimu Sheikh wa Wilaya ya KilwaKatika shindano hilo Khadija Kaudunde aliibuka na ushindi katika usomaji wa Juzuu 1, Mariam Suleiyman alishindika usomaji wa juzuu 3, Shaweji Mwichande Juzuu 5, Amir Hassan Mkwachu Juzuu 10 huku Abdallah Yusuf Kombo akifanikiwa katika usomaji wa Juzuu 30.
Zawadi mbalimbali zilitolewa kwa washindi ikiwemo magodoro, Cherehani, Radio, Baiskeli kwa washindi na walimu wao pamoja na Pesa Taslimu
Msindi wa kwanza wa kusoma Juzuu Moja ,Khadija kaundunde akisoma Quran tukufu juzuu ya 1nkatika mashindano ya kuhifadhi Quran yaliyofanyika katika viwanja vya bustan ya Benjamin Mkapa wilayani kilwa
Mshindi wa kwanza wa kusoma Juzuu 30, Abdallah Yusus Kombo, Akisoma Quran katika shindano hilo
Mkuu wa wilaya ya Kilwa Abdallah Ulega akiwapongeza majaji wa shindano hilo mara baada ya kutangaza matokeo
Mkuu wa wilaya ya Kilwa Abdallah Ulega(Mwenye koti Jeusi) akiwa katika picha ya pamoja na kamati ya maandalizi ya kusoma Quran Kilwa
Kaimu Sheikh mkuu wa wilaya ,Sheikh Muhidin Matata akiongea na waislam waliohudhuria shindano hilo kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kukabidhi zawadi
Mwenyekiti wa klabu ya waandishi wa Habari Mkoa wa Lindi, Abdulaziz Ahmeid akikabidhiwa zawadi ya Msaafu katika kuthamini mchango wa wanahabari katika shindano hilo.
Mkuu wa wilaya ya Kilwa Abdallah Ulega akihutubia waislamu wa kilwa waliohudhuria katika shindano la kuifadhi na kusoma Quran
Baadhi ya washiriki wa shindano hilo
Waumini mbalimbali wa kiislamu walioshuhudia shindano hilo
Post a Comment Blogger Facebook
Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii
Note: Only a member of this blog may post a comment.