Unknown Unknown Author
Title: RPC CUP YAANZA LINDI, MABINGWA WATETEZI MINGOYO FC WAANZA VYEMA.
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
TIMU ya kata ya Mingoyo katika Manispaa ya Lindi,imeanza vizuri mashindano ya kugombea kombe la Polisi Jamii (LINDI RPC CUP), baada ya ku...
rpc cup lindi
TIMU ya kata ya Mingoyo katika Manispaa ya Lindi,imeanza vizuri mashindano ya kugombea kombe la Polisi Jamii (LINDI RPC CUP), baada ya kuwafunga wenzao wa kata ya makonde mabao 2-1 katika mchezo wa fungua dimba.

Katika mchezo huo uliofanyika jana uwanja wa Ilulu, kata ya Mingoyo ndio ilikuwa ya kwanza kujipatia bao la kuongoza na kufutia machozi, lililofungwa na Ushuru Ally, katika dakika ya 17 kipindi cha kwanza kwa shuti kali lililomshinda nguvu mlinda mlango Nyungwa Mohamedi.

Baada ya goli hilo kufungwa vijana wa Mingoyo waliliandama lango la wapinzani wao na katika dakika ya 24 mchezaji Afidhi Mohamedi alifanyiwa madhambi ndani ya eneo la adhabu na mwamuzi, Seif Ramadhani kuamuru ipigwe penati.

Aidha, penati hiyo iliyopigwa na mchezaji Hamisi Rashidi ilidakwa kistadi mkubwa na mlinda mlango wa Makonde FC, Abdu Saidi.

Vijana wa Makonde hawakukata tamaa, kwani katika dakika ya 33, mchezaji
Selemani Mazengo, aliwainua wapenzi vitini kwa kufunga bao safi la kichwa, baada ya kupokea pasi ya juu kutoka kwa, Hamisi Rashidi, na kudumu hadi mapumziko.

Kipindi cha pili kila timu iliingia uwanjani ikiwa na nguvu mpya kufuatia mawaidha waliyoyapata kutoka kwa walimu wao, hata hivyo mawaidha hayo yaliwasaidia zaidi vijana wa kata ya Mingoyo, kwani katika dakika ya 78 Afidhi Mohamedi aliifungia Mingoyo bao la pili na la ushindi, baada ya kuunganisha mpira wa mchezaji mwenzake Juma
Selemani.
rpc cup lindi
Kamanda Renatha Mzinga Akikagua Timu kabla ya Mechi ya Fungua Dimba Kuanza Ndani ya Uwanja wa Ilulu.

Akizindua mashindano hayo, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Lindi, Kamishna msaidizi Renatha Mzinga alitoa wito kwa wanamichezo ikiwemo jamii za Mkoa huo kuhusiana na Michezo

Mashindano hayo yakishirikisha timu za kata 15 za manispaa ya Lindi yana lengo la kuchagua timu itakayoundwa kushiriki katika hatua ya fainali itakayoshirikisha timu itakayochaguliwa na kila wilaya katika mkoa wa Lindi.
Makonde Fc RPC Cup Lindi
Kikosi Cha Timu ya Makonde Fc kilichocheza mechi ya Ufunguzi wa Kombe la RPC CUP Mkoa wa Lindi katika Uwanja wa Ilulu. 
Mingoyo Fc RPC Cup Lindi
Kikosi cha Timu ya Mingoyo Fc kilichocheza mechi ya Ufunguzi wa Kombe la RPC CUP Mkoa wa Lindi katika Uwanja wa Ilulu. 
Waamuzi RPC Cup Lindi
Safu ya Waamuzi waliochezesha Mchezo wa Ufunguzi wa Kombe la RPC CUP Mkoa wa Lindi katika Uwanja wa Ilulu.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top