Unknown Unknown Author
Title: EXCLUSIVE : DIAMOND AMPA MAMA YAKE GARI KAMA ZAWADI IKIWA LEO NI SIKU YAKE YA KUZALIWA. VIDEO HII HAPA
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Ingawa hayupo Tanzania lakini hakungoja mpaka arudi ndipo akabidhi zawadi hii badala yake alichokifanya ni mara baada ya kukamilisha kila...
Ingawa hayupo Tanzania lakini hakungoja mpaka arudi ndipo akabidhi zawadi hii badala yake alichokifanya ni mara baada ya kukamilisha kila kitu kinachoihusu gari hii Diamond Platnumz aliwapatia mameneja wake kwa ajili ya kuiwasilisha kwa mama yake.
zawadi ya diamond kwa mama yakeNi Toyota Lexus New Model ambapo Babu Tale amesema imegaharimi milioni 38.1 ambapo milioni 35 imetumika kulinunulia gari hilo mpaka kuingia Tanzania na Milion 3.1 imetumika kulipamba na kuweka Music System pamoja na seat Cover.
Zawadi hii ameitoa Diamond kwa mama yake kama zawadi kwa ajili ya kuadhimisha siku yake ya kuzaliwa kwa mama yake ambaye amesema ametimiza miaka 55, mama yake amesema hakutegemea zawadi hii na anamuombea mwanae kwa Mungu afanikiwe zaidi.
zawadi ya diamond kwa mama yakeBaada ya kufuturu Meneja wa Diamond Babu Tale alitangaza utaratibu wa kuzindua kwanza video mbili za Diamond kwa watu waliokuwepo hapo kisha utaratibu mwingine ukaendelea ikiwemo kumuimbia mama yake Diamond kisha kukabidhiwa gari yake.
zawadi ya diamond kwa mama yakeHii ni Kipande cha Video wakati wa mama yake Diamond anakabidhiwa gari hiyo mbele ya mastar kadhaa akiwemo Wema Sepetu, Shettah, Madee, Profesa Jay, Aunt Ezekiel na wengine kibao.
HABARI HII KWA USHIRIKIANO WA MILLARD AYO.COM na BONGOCLANTZ.COM

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top