Meneja wa mfuko wa taifa wa bima ya afya mkoa wa Lindi Fortunata Raymond,akitoa elimu kwa viongozi na wawakilishi wa Talgwu ngazi ya kata na mkoa,kuhusu faida za kuwa mwanachama wa NHIF na mfuko wa afya ya jamii CHF kwenye ukumbi wa kanisa katoliki la Mt. Francisi Axvery mkoani Lindi.
Mgeni rasmi kwenye kikao kilichoambatana na mafunzo ya mfuko wa taifa wa bima ya afya mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Lindi Vijijini bi Oliver Vavunge,ambapo aliwataka wawakilishi wafanyakazi kuwakumbusha kutimiza wajibu ili maslai yaweze kuboreka sanjari na kusisitiza kuwa watambue NHIF ina msaada mkubwa kwao na kwetu kama waajiriwa hivyo watumishi wa sekta ya afya wana jukumu kubwa la kusimamia huduma ili ziboreke zaidi kupitia fedha zinazolipwa kupitia bima ya afya,kushoto ni mwenyekiti Talgwu mkoa wa Lindi.
Katibu wa Kamati ya uratibu Talgwu Mkoa wa Lindi ndg kambogoro Rashidi akitoa taarifa ya madhumuni ya mkutano wa mwaka wa viongozi na kamati ya uratibu na utoaji wa elimu kutoka NHIF kwa mgeni rasmi ambaye ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Lindi Vijijini Oliva Vavunge.
Washiriki wakimsikiliza kwa makini hayupo pichani meneja wa mfuko wa Taifa wa bima ya afya mkoa wa Lindi Bi Fortunata Raymond,ambapo aliweka bayana makusudio ya ofisi ya Mkoa wa Lindi ilivyoweka mkakati wa kutoa elimu inayohusu umuhimu na faida za kujiunga na mifuko ya afya ya jamii(CHF), sanjari na maboresho ya kitita cha mafao cha NHIF kwa viongozi wa vyama vya wafanyakazi mkoani Lindi.
Post a Comment Blogger Facebook
Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii
Note: Only a member of this blog may post a comment.