Bondia wa ngumi za kulipwa anayeshikilia mkanda wa WBF, Francis Cheka, amepandishwa kizimbani katika mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa Morogoro, akikabiliwa na shtaka la shambulio la kudhuru mwili na kujeruhi.
Cheka amefikishwa leo kwa mara ya kwanza katika mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa Morogoro, na kusomewa shtaka, na mwendesha mashtaka wa polisi, Aminata Mazengo, mbele ya hakimu wa mahakama hiyo Said Msuya, akidaiwa mnamo julai 02 mwaka huu, bila halali na akijua kufanya hivyo ni kosa kisheria, amempiga kwa ngumi maeneo ya kichwani na tumboni, Bahati Kabanda maarufu kama Masika, na kumsababishia maumivu makali.Cheka anadaiwa kutenda kosa hilo kwa kabanda ambaye alikuwa ni meneja wa baa yake ya Vijana Social iliyopo sabasaba katika manispaa ya Morogoro baada ya kudaiwa kutoridhishwa na mahesabu ya mauzo, ambapo mahakama ilitoa masharti ya dhamana, ikimtaka kuwa na wadhamini wawili kwa kila mmoja kuweka dhamana ya maandishi ya shilingi milioni moja, ama aende rumande, ambapo Francis Cheka alikamilisha taratibu za dhamana na sasa yupo nje kwa dhamana hiyo.
About Author
JE, UNA HABARI, PICHA, TANGAZO, MAKALA NA USHAURI? USISITE KUWASILIANA NASI SIMU / WHATSAPP NAMBA 0625535420.
Advertisement
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment Blogger Facebook
Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii
Note: Only a member of this blog may post a comment.