Unknown Unknown Author
Title: BI SOMOE MOHAMEDI AMBAYE NI MLEMAVU ANAOMBA MSAADA
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Na Abdulaziz Video,Lindi Serikali imeombwa kutenga bajeti kwa watu wenye mahitaji maalumu  ikiweko wenye ulemavu na magonjwa ya kudumu s...
msaada
Na Abdulaziz Video,LindiSerikali imeombwa kutenga bajeti kwa watu wenye mahitaji maalumu ikiweko wenye ulemavu na magonjwa ya kudumu sambamba na kuwa na kampeni za huduma za Afya vijijini ili kuokoa jamii zisizo na uwezo.

Ombi hilo limetolewa na baadhi ya wananchi walioguswa na hali ya ugonjwa alionao Bi Somoe Mohamed mkazi wa kiiiji cha Mnamba, Namupa Lindi vijijini anaesumbuliwa na uvimbe usoni huku akiwa mlemavu wa macho.
msaada
Bw FILBERT MANGANYA -MKAZI WA DAR alieleza kuwa ni jukumu letu sisi wanajamii kuguswa na tatizo hilo ambapo tuna wajibu wa kutoa msaada wa kukimu maisha yake kila siku.

Nae Bi Aluiya Herode kwa upande alieleza masikitiko yake kufuatia mama huyo kukimbiwa na mumewe baada ya kupata ugonjwa huo na kutoa wito kwa akina mama kujitolea katika kumpa matunzo mama huyo ambae ana watoto 4 wanaomtegemea.

Awali akiongea na mwandishi wetu, Bi Somoe alisema kuwa licha ya tatizo alilonalo pia amesikitishwa na wanajamii wa eneo lake kutomuweka katika mpango wa tasaf wa kusaidia kaya masikini licha ya hali aliyonayo ikiwemo kutoona huku akitegemewa na watoto wakeLicha kuwa na hali hiyo aliyodumu nayo kwa zaidi ya miaka 20.
msaada
Changamoto kubwa ni kupata uhakika wa chakula na malazi huku akilea watoto wake walioshi bila kupata elimu kutokana na kushindwa kumudu na wakati mwingine kulala bila ya uhakika wa kula.
"Jamani ndg zangu hakika nateseka kama mnavoniona nimezunguka Nyangao na Ndanda kupata matibabu ila Tayari madaktari wameniambia kuwa hakuna ujanja wa matibabu kwa kuwa nasumbuliwa na Kansa nami Namuomba Mungu hadi siku atakayopenda, mtihani mkubwa ni jinsi ya kuishi Wazazi wangu wamefariki na mume wangu kanikimbia kaniachia watoto"alimalizia Bi Somoe

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top