Kila Kombe la Dunia lina taswira yake ya kipekee. Tarswira hiyo huoneshwa kupitia nembo maalum. Nembo hiyo rasmi ya Kombe la Dunia huwakilisha michuano yenyewe na nchi inayoandaa michuano hiyo kwa dunia.
Nembo rasmi ya Kombe la Dunia Brazil 2014 inajulikana kama "Kuhamasisha". Nembo hiyo ina picha ya mikono mitatu inayounda mfano wa Kombe la Dunia. Mikono hiyo mitatu ina rangi za manjano na kijani. Rangi hizi zinatoa ishara kuwa Brazil inakaribisha Ulimwengu mzima nchini humo.
Nembo hiyo imechaguliwa na jopo la wataalam, ambao walipitia nembo nyingine zipatazo 25 zilizopendekezwa na taasisi mbalimbali nchini Brazil.
ZIMESALIA SIKU MBILI KABLA YA KOMBE LA DUNIA KUANZA KUTIMUA VUMBI NCHINI BRAZIL,
Je wewe ni Timu Gani? Mimi yangu Ni Uholanzi watoto wa Van Gall
Post a Comment Blogger Facebook
Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii
Note: Only a member of this blog may post a comment.