Domayo amesaini Azam FC baada ya kumaliza Mkataba wake wa miaka miwili na Yanga SC, ambayo alijiunga nayo akitokea JKT Ruvu miaka miwi iliyopita.
Katibu wa Azam FC, Nassor Idrisa Mohamed ‘Father’ amesema katika kuendelea kukiimarisha kikosi chao kwa ajili ya msimu ujao wamepiga hatua nyingine kwa kumsaini “Kama unavyojua, baada ya kumaliza msimu vizuri tukiwa mabingwa wa Bara, tuligundua mapungufu kwenye kikosi chetu na kwa ushauri wa mwalimu wetu (Joseph Marius Omog) ndiyo tunayafanyia kazi,”alisema Father.
Domayo anakuwa mchezaji wa wa pili ndani ya siku mbili kusajiliwa na Azam FC kutoka mabingwa wa zamani na mabingwa wa kihistoria Tanzania Bara, Yanga SC baada ya jana klabu hiyo kumsaini mshambuliaji Mrundi Didier Kavumbangu.
>> BIN ZUBERY
Post a Comment Blogger Facebook
Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii
Note: Only a member of this blog may post a comment.