PICHA CHAFU ZAMFANYA RIHANNA KUWA HATIANI KUFUNGIWA ACCOUNT,TAZAMA HAPA

Rihana
Kwa Rihanna hua sio ‘big deal’ kupost picha za utupu katika mitandao ya kijamii, inavyoonekana ni moja ya starehe zake ambazo zimeonekana kuvuka mipaka iliyowekwa na wamiliki wa mtandao wa kushare picha wa Instagram.

Mwimbaji huyo wa Barbados, jana aliweka picha za utupu katika mtandao wa Instagram, lakini wamiliki wa mtandao huo waliziondoa picha hizo kwasababu zilikiuka masharti yanayozuia watumiaji kutoweka picha za aina hiyo katika mtandao huo.

Chanzo kiliuambia mtandao wa TMZ kuwa Instagram licha ya kuziondoa picha hizo pia walimtumia barua pepe ya kumuonya vinginevyo watamfungia kutoutumia mtandao huo.

Hata hivyo Riri bado aliendelea kupost picha hizo katika mtandao wa Twitter.

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post